Hakimu Mkazi Kisutu
WAKAZI
wawili wa Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu kwa ajili ya hapo baadae kuja kuunganishwa katika kesi ya wizi
wa Paspoti 26 inayomkabili Msainii wa Muziki wa asili, Chingwele Che
Mundugwao (pichani) na wenzake wanne.
Wakili wa serikali Aidah
Kisumo mbele Hakimu Mkazi Sundi Fimbo aliwataja washitakiwa hao
walifikishwa jana kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na
makosa yanayofanana ambayo yanamkabili Chemundugwao na wenzake ni Rajab
Momba na Haji Mshamu.
Akiwasomea mashitaka Momba na Mshamu,
Wakili Kisumo alidai kuwa tarehe isiyofahamika washitakiwa walikula
njama ya kutenda kosa. Aidha tarehe tofauti Dar es Salaam, Momba aliiba
hati ya kusafiria yenye namba AB 651926 mali ya serikali.
Alidai
Momba, Mshamu na Iqbal wanadaiwa tarehe isiyofahamika Dar es Salaam,
walighushi hati ya kusafiria yenye namba hiyo, kuonesha ni halali na
imetolewa na Idara ya Uhamiaji ya Tanzania jambo ambalo si kweli.
Mbali na Che mundugwao washitakiwa hao wataunganishwa na Raia wa
Uingereza Ahsan Iqbal au Ali Patel, Ofisa Ugavi wa Idara ya Uhamiaji
Shemweta Kiluwasha, Injinia Keneth Pius wa Kikosi cha Zimamoto na
Uokoaji na mfanyabiashara Ally Jabir.
Hata hivyo washitakiwa
hao walikana mashitaka na kurudishwa rumande kwa kuwa Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP),Dk.Eliezer Feleshi aliwasilisha hati ya kuwafungia
dhamana washitakiwa hao wawili kama alivyofanya kwa kina Chemunduwao na
wenzake na kwamba upelelezi bado haujakamilika na kesi itatajwa tena
Julai 22, mwaka huu, ili waunganishwe na Chemundugwao ambapo kesi yao
nayo imepangwa kuja kutajwa Julai 22 mwaka huu.
Juni 3 mwaka huu,
Chemundugwao na wenzake walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo
wakikabiliwa na makosa mbalimbali yakiwemo kosa la wizi wa paspoti 26,
ambapo hata hivyo DPP aliwasilisha hati ya kuwafungia dhamana ambapo
hadi sasa wapo gerezani.
No comments:
Post a Comment