Friday, 16 August 2013

MZEE RAPAHAEL KUBAGA







 MZEE RAPAHAEL KUBAGA




PICHA YA PAMOJA


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uhamiaji Tanzania Wakati wa Uhuru upande wa kushoto Mzee Papael kubaga akifuatiwa na  Ogastino Kubaga (Mtoto wake wa Kwanza) yupo nyuma ya Baba yake, Upande wa kulia ni  Rafael Kubaga(Kivugu) wakiwa katika sura za furaha na katika picha ya Pamoja katikati ni Mabunti zake wawili:
 Betty Kubaga,  Suzana Kubaga….
 akiwa na familia yake nyumbani kwake Chang’ombe Dar-Esa-Salaam

Katika wakati wake alipokuwa Mkurugenzi wa Uhamiaji alitoa mchango mkubwa katika fani ya michezo , na alisisitiza michezo Idarani kama vile Mpira wa miguu, Mchezo wa Ngumi, Mchezo wa mpira wa Pete, Mpira wa kikapo, bila kuwasahau Wanariadha  na idara ilijizolea sifa nyingi kutokana na michezo wanariadha wengi wazuri walikuwa wakitokea katika idara ya Uhamiaji  na hata hivyo wachezaji wa idara walisubutu kuwakilisha inchi nje ya nchi na kufanya vizuri na vijana wengi wali faidika kupitia michezo na kwasasa wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika nchi hii katika maswala ya kiulinzi na usalama

TUNASEMA TUNAKUSHUKURU
NA

” TUNAMKUMBUKA MZEE WETU KWA MALEZI YAKE MAZURI KWA IDARA”

KWETU TANGA. BLOG


Vurugu Bagamoyo




Vurugu Bagamoyo zajeruhi,

 nyumba zachomwa moto



. Madereva wa malori (fuso) na wananchi wamezusha vurugu kubwa Kitongoji cha Kweishala (Mnara wa Voda), Kata ya Mbwewe Wilaya ya Bagamoyo na kusababisha watu kujeruhiwa huku nyumba zaidi ya sita, hoteli ndogo na pikipiki moja kuteketezwa  kwa moto, na baadhi ya wanakijiji wakidaiwa kukimbia makazi yao wakihofia kuuawa.
Vurugu hizo zilianza alfajiri Agosti 15 baada ya gari aina ya Fuso liliokuwa limebeba shehena ya marobota 189 ya nguo za mitumba na 68 ya viatu kuacha njia na kupinduka  eneo la kijiji hicho, ambapo baadhi ya wakazi wa eneo hilo walivamia gari hilo na kudaiwa kupora mizigo na kuihifadhi katika nyumba zao.
Baada ya tiko hilo, Polisi wa Kituo cha Chalinze walilazimika kwenda kuongeza nguvu kutuliza ghasia hizo kutokana na wenzao wa Kituo cha Mbwewe kuzidiwa.
Katika vurugu hizo kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 15 alijeruhiwa na polisi walifanikiwa kukamata watu watatu waliohusika na tukio hilo.
Diwani wa  Kata ya Mbwewe, Omar Mhando na Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Mashaka Kigoko walisema baada ya Fuso hilo kuanguka, lililala katikati ya barabara na kusababisha magari mengine yaliyokuwa yakisafiri katika barabara kuu ya Chalinze-Segera kushindwa kuendelea na safari kwa zaidi ya saa nne, hali ambayo iliwalazimu madereva kujikusanya pamoja ili kuwapa msaada wenzao.
“Chanzo cha huu mkasa ni hilo Fuso lililoanguka na shehena ya mitumba na viatu, ilikatisha barabara na kuziba njia hivyo magari mengine yalipofika hapo yalikwama, na muda ulivyozidi waliamua kushuka na kufuatilia kulikoni na kukuta wenzao wamepata ajali,lakini badala ya kusaidiwa kutoka garini watu walivamia na kupora mali,” alisema Mhando.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi amethibitisha tukio hilo na  kuwa hadi saa tisa alasiri jana wanakijiji sita ndiyo walioripotiwa kujeruhiwa.

Thursday, 15 August 2013

RC TANGA AMUWEKA MAHABUSU MKAGUZI WA NDANI

RC TANGA AMUWEKA MAHABUSU MKAGUZI WA NDANI

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni Mtaafu Chiku Gallawa, amemuweka rumande Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Najim Mpate, kwa madai ya kumdharau wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Tukio hilo lilitokea jana wakati Mpate alipokuwa anatoa maelezo kufuatia hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Halmashauri ya Pangani ambapo ilionekana kuna hoja ambazo hazijapatiwa majibu tangu mwaka wa fedha 2008/2009.

Hoja kuu inayoongelewa ni ile inayohusu mkandarasi mmoja aliyelipwa fedha zaidi ya mkataba ulivyokuwa unaonyesha hivyo Mkuu wa Mkoa alikuwa anataka maelezo kwa nini hoja hiyo ya karibu miaka mitano iliyopita inaendelea kujirudia na kwanini mkandarasi husika hajarudisha fedha hizo ili kufuta hoja hiyo.

Mara baada ya kujieleza Mkaguzi huyo alilipiga chini kabrasha alilokuwa amelishinda, kitendo ambacho kiliwashtua madiwani kwani kilionekana kuwa ni dharau ya wazi kwa Mkuu wa Mkoa.

Baada ya tukio hilo, hilo Mheshimiwa Gallawa alisikika akisema, “Hivi huyu ni nani mbona amekaa kijeuri. Kwanza unajibu maswali kijeuri, lakini mimi ni mtu wa kunitupia faili chini” Hii ni halmashauri yako? OCD mchukue huyu mtu ukampumzishe.”
Akieleza baada ya kuisha kikao, Mheshimiwa Gallawa alisema yeye ndiye anawajibika HAlmashauri zinapokuwa na hoja zilizokosa majibu na hivyo hatakubali wazembe wachahce kwenye halmashauri wamharibie dhamana aliyopewa ya kuwatumikia wananchi.”
RC TANGA AMUWEKA MAHABUSU 
MKAGUZI WA NDANI



Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni Mtaafu Chiku Gallawa, amemuweka rumande Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Najim Mpate, kwa madai ya kumdharau wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Tukio hilo lilitokea jana wakati Mpate alipokuwa anatoa maelezo kufuatia hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Halmashauri ya Pangani ambapo ilionekana kuna hoja ambazo hazijapatiwa majibu tangu mwaka wa fedha 2008/2009.

Hoja kuu inayoongelewa ni ile inayohusu mkandarasi mmoja aliyelipwa fedha zaidi ya mkataba ulivyokuwa unaonyesha hivyo Mkuu wa Mkoa alikuwa anataka maelezo kwa nini hoja hiyo ya karibu miaka mitano iliyopita inaendelea kujirudia na kwanini mkandarasi husika hajarudisha fedha hizo ili kufuta hoja hiyo.

Mara baada ya kujieleza Mkaguzi huyo alilipiga chini kabrasha alilokuwa amelishinda, kitendo ambacho kiliwashtua madiwani kwani kilionekana kuwa ni dharau ya wazi kwa Mkuu wa Mkoa.

Baada ya tukio hilo, hilo Mheshimiwa Gallawa alisikika akisema, “Hivi huyu ni nani mbona amekaa kijeuri. Kwanza unajibu maswali kijeuri, lakini mimi ni mtu wa kunitupia faili chini” Hii ni halmashauri yako? OCD mchukue huyu mtu ukampumzishe.”

Akieleza baada ya kuisha kikao, Mheshimiwa Gallawa alisema yeye ndiye anawajibika HAlmashauri zinapokuwa na hoja zilizokosa majibu na hivyo hatakubali wazembe wachahce kwenye halmashauri wamharibie dhamana aliyopewa ya kuwatumikia wananchi.”

CCM Taifa yapinga madiwani Bukoba Mjini kutimuliwa


CCM Taifa yapinga madiwani 

Bukoba Mjini kutimuliwa



Dar es Salaam. Siku moja baada ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kagera kuwatimua madiwani wanane, chama hicho ngazi ya Taifa kimetengua uamuzi huo.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Averin Mushi juzi alitangaza uamuzi wa kuwatimua madiwani hao kwa kile alichosema ni kwa ajili ya masilahi ya chama na wananchi wa Bukoba.
Madiwani waliotimuliwa ni; Yusuph Ngaiza ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba na Diwani wa Kashai wakati wengine ni; Samwel Ruhangisa (Kitendagulo) na Robart Katunzi wa Hamugembe.
Wengine waliorushiwa virago ni; Deus Mutakyahwa (Nyanga), Richard Gasper (Miembeni), Mulungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda (Buhembe), ambaye pia alikuwa Naibu Meya na Dauda Kalumuna aliyekuwa Diwani wa Ijuganyondo.
Mushi alisema; kwa mujibu wa Ibara ya 93, kifungu cha 15, inakipa kikao hicho mamlaka ya kuwatimua uanachama na kwamba pamoja na kukaidi maelekezo mbalimbali ya chama hicho, pia wameendelea kushirikiana na upinzani kuhujumu chama.
Tamko la CCM Taifa
Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM, Nape Nnauye alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa chama chake kimetengua uamuzi uliotolewa na Halmashauri hiyo ya Kagera kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kukaidi maelekezo mbalimbali ya chama hicho.
Nnauye alisema; kutokana na utaratibu wa CCM na hayo yaliyotokea, uamuzi ni kwamba; madiwani wote waliosimamishwa wanatakiwa kuendelea na kazi zao kama kawaida hadi hapo Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama itakapokutana Agosti 23 mjini Dodoma. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Nnauye alibainisha kuwa uamuzi uliotolewa na CCM Mkoa wa Kagera wa kuwasimamisha madiwani wa chama hicho kwa madai ya kukiuka taratibu za chama sio sahihi, kwani uamuzi huo unapaswa kutolewa na Halmashauri Kuu ya Chama Taifa.
Madiwani waliotimuliwa ni wale wa Manispaa ya Bukoba ambao wamekuwa wakitajwa kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki ambaye amekuwa akivutana vikali na Meya wa Manispaa hiyo, Anatory Amani.
Nnauye alisema: “Tunasema kuwa uamuzi uliotolewa na Halmashauri ya Mkoa wa Kagera, kuwafukuza madiwani nane sio sahihi kwani Kamati Kuu ya CCM ndiyo yenye uamuzi wa mwisho kwani hata mimi Nape siwezi kutoa uamuzi kama huo.
Alisema kuwa wanatambua kwamba kuna mgogoro mzito kati ya madiwani wa CCM na Meya wa Manispaa hiyo, lakini uamuzi uliotolewa wa kuwasimaimisha sio sahihi, kwani ni kwenda kinyume na taratibu za chama jambo ambalo wao wanalipinga.
Kagasheki atoa neno

Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini, Khamis Kagasheki amesema kuwa hafahamu lolote kuhusu kufukuzwa madiwani lakini anafahamu kuwapo kwa mgogoro huo.
“Ni kweli ninaufahamu mgogoro wa madiwani wangu, nilikuwa sipo wakati wanafukuzwa, lakini kwa sasa nimerudi, nitafuatilia na kulishughulikia kwa undani zaidi ili kupunguza mgogoro huo,” alisema Kagasheki.
Aliongeza, hatua zilizochukuliwa za kuwafukuza ni kinyume na taratibu,lakini atawasiliana na viongozi hao ili kujua namna ambavyo wanaweza kulitatua suala hilo kwa busara zaidi.
Alisema, mgogoro huo ni wa muda mrefu, lakini unahitaji busara wakati wa utatuzi wake, jambo ambalo linaweza kuleta umoja na mshikamano ndani ya chama.
Kinachoelezwa na Madiwani
Nnauye alisema pia kuwa wamepokea barua za madiwani hao ambao wamesimamishwa kwa madai kwamba chanzo cha kufukuzwa kwao ni kusema ukweli kuhusu utendaji kazi wa Meya huyo.
Alisema, “Kuna tuhuma za Meya kushindwa kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi ambayo ni kama ile ya Soko, maji, barabara na kituo cha daladala. CCM taifa tuna taarifa za kina kuhusu mgogoro huo kitu ambacho tutakijadili kwenye kikao cha Halmashauri kuu na kukitolea uamuzi sahihi,”alisema Nnauye.
Nnauye alibainisha kuwa kutokana na tuhuma mbalimbali zinazotolewa kwa Meya huyo CCM inafanya uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma hizo na kwamba chama kitatoa uamuzi pindi watakapo baini kuwa tuhuma zinazoelezwa kwa Meya zinaukweli au laa.
“Meya amekuwa akituhumiwa kuwa ameshindwa kusimamia na kutekeleza masuala mbalimbali kwenye Halmashauri ya mji huo kitua ambacho kinadaiwa kuleta mgogoro na madiwani ambao wanapingana naye, sasa ifahamike kuwa CCM haitamfumbia macho mtu yoyote anakwenda kinyume na taratibu tutafanya uchunguzi na kutoa maamuzi.”
Aidha alisema kuwa hawana uhakika kama kusimamishwa kwa madiwani hao taratibu zilifuatwa au laa jambo ambalo wao kama uongozi wa juu wa chama lazima walifanyie kazi ili kupata ukweli zaidi.
“Hatuna uhakika kama madiwani waliosimamishwa taratibu zilifuatwa ikiwa pamoja na kuwaita na kuwahoji kila mmoja, sisi kama Kamati Kuu tutakachokifanya lazima tuwaite kila mmoja atoe malalamiko yake ili tujue ukweli zaidi upo wapi,”alisema.
Nnauye alitoa mifano ya Halmashauri ambazo nazo zilikuwa na mgogoro kama wa Bukoba, Moshi na Kibondo, lakini yote ilimalizika na bila kuwana mvutano wa aina yeyote baada ya kufanyika kwa mikutano ya ndani.


“Ninachoweza kusema Bukoba wamekosea kutoa taarifa kwa umma, kwani jambo kama hili lilitokea Moshi na Kibondo, lakini ilimalizika kimya kimya bila hata kusambaa kwa kama ilivyo kwa Bukoba kwani njia za mikutano zilitumika kuondoa tofauti zilizokuwepo,”alisema Nnauye.
Madiwani wakwepa kuzungumza
Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Bukoba waliotimuliwa, wamekwepa kuzungumzia hatima yao wakidai madai ya kufukuzwa wameyasikia kwenye vyombo vya habari na wanasubiri barua.
Madiwani hao Gasper Richard (Miembeni),Robart Katunzi(Hamugembe)walisema wanasubiri kupewa taarifa rasmi huku Deus Mtakyahwa(Nyanga)akidai alikuwa safarini.Madiwani wengine waliopigiwa simu hawakuwa tayari kupokea wala kuzungumzia lolote kuhusu kufukuzwa kwao.
Taarifa za kutimuliwa kwa madiwani hao zilileta mshtuko mkubwa mjini hapa huku wengine wakionyesha hofu ya CCM kutetea Kata kata zote nane endapo uchaguzi utafanyika kujaza nafasi hizo.
Chadema Bukoba
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Bukoba, Victor Sherejei alidai umauzi huo ulikuwa umecheleweshwa kutokana na kuendelea kwa mgogoro baina ya madiwani hao.
Mbali na kusema kuwa mgogoro huo ulikuwa unakwamisha maendeleo ya wananchi, pia alisema chama chake kina nafasi kubwa ya kuchukua kata zote za madiwani waliokuwa wa CCM endapo uchaguzi ungerudiwa.
Imeandaliwa na Phinias Bashaya, Bukoba, Patricia Kimelemeta, Aidan Mhando na Irene Mossi, Dar.

DK. MGIMWA : SERIKALI KUCHUNGUZA HOSPITALI BINAFSI

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 DK. MGIMWA : SERIKALI KUCHUNGUZA
 HOSPITALI BINAFSI


 
 
 
Photo: DK. MGIMWA : SERIKALI KUCHUNGUZA HOSPITALI BINAFSI

Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa amesema Serikali iko katika mpango wa kuzifanyia uchunguzi hospitali binafsi zinazotoa huduma ya afya kwa gharama kubwa ingawa zinapata misamaha ya kodi mbalimbali zinapoagiza dawa na vifaa vingine vya afya.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Fedha,  Dk. William Mgimwa (pichani), alipotakiwa na waandishi wa habari kutoa msimamo wa serikali kuhusu hospitali binafsi zinazotoza fedha nyingi kwa wagonjwa.

Dk. Mgimwa alisema baada ya uchunguzi huo Serikali itachukua hatua madhubuti dhidi ya Serikali kwani ilitarajiwa kuwa kusamehewa kodi kungewanufaisha wananchi kwa kupata matibabu kwa gharama nafuu.Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa amesema Serikali iko katika mpango wa kuzifanyia uchunguzi hospitali binafsi zinazotoa huduma ya afya kwa gharama kubwa ingawa zinapata misamaha ya kodi mbalimbali zinapoagiza dawa na vifaa vingine vya afya.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (pichani), alipotakiwa na waandishi wa habari kutoa msimamo wa serikali kuhusu hospitali binafsi zinazotoza fedha nyingi kwa wagonjwa.

Dk. Mgimwa alisema baada ya uchunguzi huo Serikali itachukua hatua madhubuti dhidi ya Serikali kwani ilitarajiwa kuwa kusamehewa kodi kungewanufaisha wananchi kwa kupata matibabu kwa gharama nafuu.

RAIA WA UINGEREZA ASHIKILIWA KWA UJANGILI

 
 
 
 
 
 
 
RAIA WA UINGEREZA ASHIKILIWA
 KWA UJANGILI

 
 
 
 
 
 
Photo: RAIA WA UINGEREZA ASHIKILIWA KWA UJANGILI

Jeshi la Polisi nchini linamshikilia raia wa Uingereza kwa tuhuma za kukutwa na nyara mbalimbali za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh100 milioni, vikiwamo vipande vinane vya meno ya tembo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda MAalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ni kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafirishaji Mizigo (TALL), alikamatwa juzi saa 2:00 usiku maeneo ya Mbezi Beach, wilayani Kinondoni.
Afande Kova alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na meno 20 na kucha 22 za Simba, shanga mbalimbali zilizotengenezwa kwa meno ya tembo, Kasuku na nyara nyingine ambazo hairuhusiwi kumiliki bila kibali.

Alisema uzito wa nyara hizo ni kilo 25, walimkuta na mawe mbalimbali yanayodhaniwa ni madini sambamba na ganda moja la bomu lenye ukubwa mita 130.Jeshi la Polisi nchini linamshikilia raia wa Uingereza kwa tuhuma za kukutwa na nyara mbalimbali za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh100 milioni, vikiwamo vipande vinane vya meno ya tembo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda MAalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ni kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafirishaji Mizigo (TALL), alikamatwa juzi saa 2:00 usiku maeneo ya Mbezi Beach, wilayani Kinondoni.
Afande Kova alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na meno 20 na kucha 22 za Simba, shanga mbalimbali zilizotengenezwa kwa meno ya tembo, Kasuku na nyara nyingine ambazo hairuhusiwi kumiliki bila kibali.

Alisema uzito wa nyara hizo ni kilo 25, walimkuta na mawe mbalimbali yanayodhaniwa ni madini sambamba na ganda moja la bomu lenye ukubwa mita 130.
 
 
 

Wednesday, 14 August 2013

Mamlaka ya Maji Tanga yapewa agizo maalumu



Mamlaka ya Maji Tanga

 yapewa agizo maalumu




Tanga.Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Maji taka jijini Tanga (Uwasa) jana ilizinduliwa rasmi na kutakiwa iongeze ufanisi ili iendelee kuwa miongoni mwa Mamlaka bora za mfano mzuri nchini.
Bodi hiyo itaongozwa wa Salum Shamte ambaye ni Mwenyekiti baada ya kuchukua nafasi ya Raymond Mhando ambaye aliiongoza tangu Agosti mwaka 2010 hadi Juni 2013.
Akizungumza wakati akizindua bodi hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego alisema bodi hiyo mpya ina jukumu la kuhakikisha inaimarisha majukumu yaliyoachwa na bodi iliyomaliza muda wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwasa, Joshua Mgeyekwa alisema wakati wa hafla hiyo kuwa Mamlaka hiyo ni bora na ya mfano nchini ambapo inatoa huduma ya majisafi kwa wakazi 262,398 ambao ni asilimia 96 ya wakazi wote wa Jiji la Tanga.
Kwa upande wa huduma ya majitaka Mamlaka hiyo inahudumia watu 26,520 ambao ni asilimia 9.7 ya wakaz.