KWA MISINGI YA DINI
Akizungumza katika Baraza la Eid El Fitr mjini Tabora jana, Makamu wa
Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal amesema “ni busara waumini wa dini na
madhehebu kujenga utamaduni wa kuvumiliana hasa zinapotokea hitilafu
miongoni na kati yao. Ubaguzi unaotokana na kabila, rangi, jinsia au
mahala mtu alipo au anapotoka nii lazima kuukemea na kuukataa kwa nguvu
zetu zote.”.
“Kaeni pamoja na kutafuta muafaka kwa njia ya
majadiliano ya amani na upendo, pasipo kutawaliwa na jazba wala chuki.
Tukumbuke kauli na angalizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba vita ya dini
haina mshindi,” alisema.
Alisema anaamini viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kusaidia kujenga
maadili mema katika taifa hili na kwamba watu wakishiba imani ndani ya
nafsi zao, wakaelewa na kuzingatia mafundisho ya dini zao, maovu
yataondoka kati yao.
Aidha Dr. Bilal alisema “kuwepo kwa amani
na utulivu unaifanya serikali kupata ahueni, kwamba badala ya kutenga
bajeti kubwa kupanua magereza, kugharamia wafungwa na mahabusu na
uendeshaji wa mahakama, rasilimali hizo zitaelekezwa katika mipango
mingine ya maendeleo.”
Dk. Bilal alisema katika siku za hivi
karibuni, yameibuka matukio kadhaa yanaoashiria kutaka kuvuruga amani na
utulivu wa taifa na kwamba hujuma hizo zinafanywa na watu wachache
wasiolitakia mema taifa kwa maslahi yao binafsi.
Aliongeza kuwa
“kamwe serikali haitakuwa tayari kuona Mtanzania anaishi kwa hofu na
mashaka ndani ya nchi yake kutokana na vitendo vya wahuni wachache. Kila
itakapobidi, tutawasaka, tutawakamata na kuwakomesha kwa rungu la mkono
wa sheria. Nawahakikishieni kwamba Tanzania yetu itabaki nchi salama ya
amani na utulivu na ya kupigiwa mfano daima.”
Alisema uhuru wa
kuabudu katika taifa hili umejengewa misingi ndani ya katiba na
kutokana na ukweli huo, kila mmoja anapaswa kuheshimu imani au dini ya
mwenzake pasi kujiona kwamba imani au dini yake ni bora zaidi.
KWA MISINGI YA DINI
Akizungumza katika Baraza la Eid El Fitr mjini Tabora jana, Makamu wa
Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal amesema “ni busara waumini wa dini na
madhehebu kujenga utamaduni wa kuvumiliana hasa zinapotokea hitilafu
miongoni na kati yao. Ubaguzi unaotokana na kabila, rangi, jinsia au
mahala mtu alipo au anapotoka nii lazima kuukemea na kuukataa kwa nguvu
zetu zote.”.
“Kaeni pamoja na kutafuta muafaka kwa njia ya majadiliano ya amani na upendo, pasipo kutawaliwa na jazba wala chuki. Tukumbuke kauli na angalizo la Rais Jakaya Kikwete kwamba vita ya dini haina mshindi,” alisema.
Alisema anaamini viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kusaidia kujenga maadili mema katika taifa hili na kwamba watu wakishiba imani ndani ya nafsi zao, wakaelewa na kuzingatia mafundisho ya dini zao, maovu yataondoka kati yao.
Aidha Dr. Bilal alisema “kuwepo kwa amani na utulivu unaifanya serikali kupata ahueni, kwamba badala ya kutenga bajeti kubwa kupanua magereza, kugharamia wafungwa na mahabusu na uendeshaji wa mahakama, rasilimali hizo zitaelekezwa katika mipango mingine ya maendeleo.”
Dk. Bilal alisema katika siku za hivi karibuni, yameibuka matukio kadhaa yanaoashiria kutaka kuvuruga amani na utulivu wa taifa na kwamba hujuma hizo zinafanywa na watu wachache wasiolitakia mema taifa kwa maslahi yao binafsi.
Aliongeza kuwa “kamwe serikali haitakuwa tayari kuona Mtanzania anaishi kwa hofu na mashaka ndani ya nchi yake kutokana na vitendo vya wahuni wachache. Kila itakapobidi, tutawasaka, tutawakamata na kuwakomesha kwa rungu la mkono wa sheria. Nawahakikishieni kwamba Tanzania yetu itabaki nchi salama ya amani na utulivu na ya kupigiwa mfano daima.”
Alisema uhuru wa kuabudu katika taifa hili umejengewa misingi ndani ya katiba na kutokana na ukweli huo, kila mmoja anapaswa kuheshimu imani au dini ya mwenzake pasi kujiona kwamba imani au dini yake ni bora zaidi.