TANGA KWDETU |
TANZIA
"Kwa ishirikiano wa Bliog za Tanga Kwetu, Zigua Simo na njero, Boshazi ondeZigua, Samba na Baragumu ya Mnyonge....wamestushwa na kifo cha Kamanda "
GEORGE JOHN LAIZER
Che.Andrew Kizenga Shundi |
kwani Tarehe 17/09/2013 alitembelea BUGANGO BORDER na kuahidi yakuwa atakapo pata nafasi atatembelea eneo hili tena na kusema yakuwa alikuwa akisikia kituo hiki cha Bugango sasa leo amefika ...akasema kwakweli mimi siamini nitarudi tena....mwisho wa kauri yake kwakweli sisi wana bugango tunamuomboa apumzike mahali pema peponi..Amin
- MPIGANAJI AFIA 'VITANI' AKILITETEA TAIFA LAKE
- AMEACHA MKE NA WATOTO WAWILI.
- AFISA UHAMIAJI MKOA WA KAGERA AONGOZA WAOMBOLEZAJI
Idara ya Uhamiaji mkoa wa Kagera imekumbwa na simanzi na
majonzi makubwa baada ya kumpoteza askari wake Mkaguzi wa Uhamiaji George John
Laizer aliyefariki jana katika kituo cha Afya Bunazi wilayani Missenyi
akisubiri matibabu.
Marehemu Laizer alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari
ambapo inasemekana siku mbili kabla ya kifo chake alikuwa akiugua typhoid. Baada
ya kwenda kituoni hapo kutibiwa hali yake ilibadilika ghafla jana asubuhi hali
iliyopelekea akimbizwe kituo cha Afya kwa matibabu. Akiwa kituoni hapo, ndipo
alipokata roho na kuiga dunia.
Marehemu Laizer ni mzaliwa wa mkoa wa Arusha mwaka
1970, alipata elimu ya msingi katika shule ya Mchombe mkoani Morogoro
kuanzia mwaka 1979 hadi 1985. Mwaka 1986 hadi 1989 alipata elimu ya sekondari
katika shule ya Vunjo.
Mnamo tarehe 12/12/1990, aliajiriwa rasmi kuwa afisa
uhamiaji mara baada ya kumaliza mafunzo ya awali katika chuo cha polisi Moshi
na kupangiwa kufanya kazi katika kituo cha Holili mkoa wa Kilimanjaro.
Marehemu ameacha mke na watoto wawili.Leo asubuhi mjini Bukoba katika
ofisi za uhamiaji, Afisa Uhamiaji mkoa wa Kagera DCI. George Kombe
aliongoza maofisa mbalimbali kutoka vyombo vya ulinzi na usalama na
asasi za kiraia katika kuuaga mwili wa marehemu ambapo baadaye majira ya
saa tano na nusu asubuhi ulisafirishwa kwenda Rusumo ambako huko pia
ataagwa na hatimaye kusafirishwa nyumbani kwao mkoani Arusha kwa
mazishi.
Blogu ya Bugango
inaungana na wana-Uhamiaji katika wakati huu mgumu wa kuomboleza kuondokewa na
kijana aliyekufa akilitumikia taifa lake katika oparesheni Kimbunga.
Askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wakitoa heshima zao za mwisho kwa Kamana Laizer leo hii mjini Bukoba |
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
Mlima kilimanjaro |