|
Simba wa Tanzania |
JWTZ kushiriki mazoezi
Angola
|
JWTZ... |
Dar es Salaam. Maofisa na Askari 35 wa Jeshi la
Wananchi (JWTZ),
kutoka Kamandi ya Jeshi la Anga wameondoka nchini jana kuelekea Angola
kushiriki mazoezi ya kijeshi ya Blue Zambezi ambayo yanatarajiwa kuanza
nchini humo leo (Agosti 20) hadi Agosti 31 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kuwaaga maofisa hao katika
Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam jana, Meja Jenerali Hassan Vuai Chema
aliwataka wanajeshi hao kuonyesha nidhamu ili kujenga ushirikiano uliopo
baina ya Tanzania na nchi zingine za Jumuia ya Mandeleo Kusini mwa
Afrika (SADC).
|
JWTZ |
“Mkiwa Angola mna jukumu la kufanya kazi kwa
bidii, kujifunza na kutoa kwa wengine kile ambacho tunacho ili wengine
wajifunze kutoka JWTZ”
alisema Meja Jenerali Chema na kuongeza kuwa
katika msafara huo kuna maafisa 21 na askari wa kawaida 14.
Alisema kuwa msafara huo utaongozwa na Brigedia
Jenerali Azra Ndimgwango na mazoezi hayo yanashirikisha vikosi vya jeshi
kutoka nchi zingine za SADC yakiwa na lengo la kuwaandaa wapiganaji hao
kutoa msaada mara nchi moja inapotokewa na majanga.
“Tunawandaa wawe tayari yanapotokea majanga kama
vile usambazaji wa chakula, dawa na vifaa vingine”
alisema na kuongeza
kuwa mafunzo hayo ambayo yatahusiaha matumizi ya helikopta katika
kukabiliana na majanga anaamini yatapanua zaidi upeo wa wanajeshi wa
nchini katika kukabiliana na majanga.
|
kwetu Tanga |