Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ilala limewasimamisha kazi watumishi
wanne wa Manispaa hiyo kwa vitendo mbalimbali vya ubadhirifu wa mali za
umma pamoja na uwajibikaji usioridhisha. Hatua hii imekuja baada ya
Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kukataa kupokea
taarifa za mapato na matumizi za Halmashauri ya Ilala baada ya kubaibni
ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni 2/=. Aidha Baraza la Madiwani
limeagiza watumishi wengine 21 kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Maamuzi hayo yalitangazwa na Meya wa Manispaa hiyo, Ndugu Jerry Silaa,
ambaye aliwataja waliosimamishwa kuwa ni mhandisi wa Manispaa ambaye
anatuhumiwa kwa kusimamia ujenzi na sheria za mipango miji. Tuhuma
nyingine za Mhandisi huyo ni pamoja na kushindwa kusimamia ukarabati wa
barabara mjini na matumizi yaayotia mashaka ya fedha za ukarabati wa
barabara, kutoa kibali cha ujenzi wa ghorofa 14 katika mtaa wa Indira
Gandhi wakati kwa mujibu wa sheria zilizopo eneo hilo inaruhusiwa
kujenga majengo yasiyozidi ghorofa 10.
Mtumishi mwingine
aliyesimamishwa ni Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa majengo kwa kushindwa
kusimamia ujenzi wa majengo kwa mujibu wa sheria zilizopo. Aidha,
anatuhumiwa kuchangia ajali ya jingo lililoanguka katika mtaa wa Indira
Gandhi na kusababisha vifo vya watu 36 na wengine kujeruhiwa. Aidha
katika watumishi ambao Baraza la Madiwani limeagiza kuwa wachukuliwe
hatua za kinidhamu ni pamoja na KAimu Ofisa elimu Sekondari na Kaimu
Ofisa Elimu Msingi katika manispaa hiyo.
No comments:
Post a Comment