Saturday, 15 June 2013

Lowassa atangaza ndoto yake


Lowassa atangaza ndoto yake

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema kuwa ana ndoto kwamba siku moja sekta ya elimu itapewa kipaumbele cha kwanza nchini na kuzikomboa rasilimali za taifa la Tanzania zinazowanufaisha wageni na kuacha wananchi wakiambulia faida kidogo.
Huku akimtaja Dk Martin Luther King aliyekuwa mwanaharakati wa haki za Wamarekani weusi aliyefariki kabla ya kuuona utimilifu wa ndoto yake, Lowassa alisema kuwa anamwomba Mungu asimwondoe duniani ili aweze kushiriki kuifanya ndoto hiyo kuwa kweli itakayokamilika siku si nyingi ambapo viongozi watakubali kuwa elimu bora ndiyo itakayowasaidia Watanzania kuchimba madini yao na kuyauza kwa faida duniani.
Akizungumza wakati wa kuchangia SACCOS ya walimu ya Moshi Vijijini, Ushirika wa Stadium jana, Lowassa alisema kuwa katika ndoto yake anawaona viongozi wakikubali kwamba elimu bora ndiyo italisaidia taifa kuumiliki utalii na kunufaika nao, badala ya kuwaachia wageni wanufaike nao, huku Watanzania tukiambulia makombo.
Wakati Lowassa akieleza ndoto yake hiyo, Mwenyekiti wa TLP na mbunge wa Vunjo Augustine Mrema amesema: “Biashara ya urais imenishinda namwachia Lowassa kwani mimi nimeamua kurudi kwenye biashara ya rejareja.”
“Ninayo ndoto kuwa siku si nyingi zijazo, elimu itapewa kipaumbele cha kwanza nchini Tanzania.
Na namwomba Mwenyezi Mungu asiniondoe duniani, kabla sijauona utimilifu wa ndoto hii kama Dk King (Martin Luther) alivyoondolewa kabla hajaiona ndoto yake ikitimia, bali namwomba anipe muda na nguvu, niweze kushiriki katika kuifanya ndoto hiyo iwe kweli,” alisema Lowassa.
Katika harambee hiyo ambapo zilipatikana jumla ya Sh1.3 bilioni , kati ya hizo fedha taslimu zilikuwa Sh250 milioni, Lowassa alifafanua kuwa itafika wakati ambapo elimu ya Tanzania itakuwa bora na kuwavutia majirani zake kuja kuwasomesha watoto wao nchini.
Akizungumzia kudorora kwa elimu nchini, Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema kuwa bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya sekta ya elimu imekuwa ikitegemea fedha za wahisani kwa asilimia 70 na kwamba jambo la kusikitisha wahisani hao hawatoi fedha zote wanazoahidi, badala yake hutoa asilimia kati ya asilimia 40 na 50 ya fedha walizoahidi.
“Bajeti yetu ya maendeleo ya sekta ya elimu kila mwaka haitekelezeki kwa upungufu wa asilimia 30-35. Kwa hali hii tutapataje maendeleo katika sekta ya elimu?” alihoji Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli mkoani Arusha na kuongeza: “Mwaka 1992 tulikuwa na Watanzania asilimia 15 tu wasiojua kusoma na kuandika, ilihali hivi sasa tuna Watanzania takribani asilimia 31 wasiojua kusoma.”
Lowassa alisema kuwa wakaguzi wa shule za msingi na sekondari kushindwa kukagua shule zote nchini huchangia kushuka kwa elimu, akibainisha kwamba asilimia 20 pekee ya shule zote ndizo hukaguliwa kwa mwaka.
Alisema ili kufikia mafanikio yatakayoletwa na elimu, Serikali inapaswa kumjali mwalimu kwa kumpa motisha na mazingira mazuri ya kufundishia.
Akijibu hoja za watu wanaosema kuwa kuboresha huduma za walimu haiwezekani kutokana na idadi yao kuwa kubwa, alinukuu sehemu ya hotuba ya Rais wa zamani wa Marekani Franklin Roosevelt akisema: “ Kitu kimoja tunachopaswa kukiogopa ni woga wenyewe.”
Lowassa alisema Watanzania wanapaswa kuuogopa woga unaowafanya waone kuwa pamoja na madini walionayo, gesi, mbuga nyingi za wanyama na ardhi nzuri ya kilimo, hawawezi kusimamia rasilimali hizo na kupata mapato makubwa yatakayowawezesha kuwalipa walimu vizuri.
Naye Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba alimuunga mkono Lowassa kwa kuitaka Serikali kuwekeze katika elimu, pamoja na kuboresha maisha ya walimu.
Akizungumzia mchango wa Lowassa katika elimu, Makamba alisema kuwa anamfahamu kiongozi huyo kama mtu asiyeogopa, huthubutu, hasa wakati aliposimamia ujenzi wa shule za sekaondari za kata nchini.
“Nakumbuka jinsi alivyompeleka mbio baba yangu Mzee Makamba alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, “alisema Makamba.
Kwa upande wake Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) alimsifu Lowassa akisema kuwa ni mchapakazi mahiri aliyefahamiana naye wakati wote walipokuwa mawaziri.
“Alipokuwa Waziri na mimi nilikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, ni hodari sana, nakuombea Mungu akujaalie katika maisha yako,” alisema Mrema.

KOMRED: Peter Shundi…..Na zilipendwa..



KOMRED: Peter Shundi…..Na zilipendwa

*      NAKUMBUSHA KATIKA MAISHA ISHI KWA AMANI, AMUA KWA BUSARA, FIKIRI KWA KINA, TENDA KWA HEKIMA, PENDA KWA DHATI, OMBA KWA IMANI, HUBIRI KWA MATENDO, ONGEA KWA NIDHAMU, TII KWA UNYENYEKEVU, ABUDU KWA ROHO NA KWELI, ENENDA KWA ROHO, TENDA KWA WAKATI, TAMBUA UWEPO WAKO, JITATHMINI UMETOKA WAPI UKO WAPI UNAENDA WAPI KIROHO, KIMWILI NA KIMAENDELEO, ZAIDI YA YOTE JIHESHIMU, JITUNZE, JIAMINI, JITAFAKARI KWANI VYOTE VINATOKANA NA JINSI WEWE ULIVYO. MUNGU NAYE YUKO PAMOJA NAWE HATA SASA NA MILELE! MUNGU AKUBARIKI, AKULINDE NA KUKUHIFADHI.

*      KWA MFANO UPO KWENYE SHEREHE, WAMEANZA KUGAWA MSOSI IMEFIKA ZAMU YAKO MSOSI UMEISHA WAKATI WA VINYWAJI MCHEZO ULEULE VINYWAJI VIMEISHA IMEFIKA WAKATI WA KUGAWA TOOTH PICKS WAKAANZIA KWAKO, KAMA INGEKUWA NDIO WEWE UNGEPOKEA AU?

*      MWALIMU: JOHN JE UNGEPENDA KUWA NANI UKIWA MKUBWA? JOHN:NINGEPENDA KUWA TAJIRI MKUBWA NIMILIKI MAGARI NA MAJUMBA YA KIFAHARI HALAFU NAOA NAKUMPANGISHIA MKE WANGU HOTELI PARIS, NAMNUNULIA MAGARI YA KIFAHARI NA KUMPELEKA KILA ANAPOTAKA: MWALIMU AKAGEUKA UPANDE WA PILI "EEEH NA WEWE DORIN UNAPENDA KUWA NANI BAADAE? DORIN: NATAKA KUWA MKE WA JOHN. MWALIMU HOI! "CHEZEA WATOTO WA DIGITAL WEWE' USIKU MWEMA...!.

*      KILA UKUTANAPO NA UGUMU WA MAISHA. TUMIA MUDA HUU POPOTE PALE UENDAPO. MUNGU AKUJALIE KINGA KWA KILA JARIBU, MSAMAHA KWA KILA KOSA, MATUMAINI KWA KILA LENGO, JIBU KWA KILA OMBI, "UPENDO KWA WATU WOTE" NAWATAKIA USIKU MWEMA...!

*      TAFAKARI....! WANAFUNZI AMBAO WALIANZA DARASA LA KWANZA MWAKA 2002 NI WANAFUNZI AMBAO WANA BAHATI SANA...! WALIPOANZA SHULE TU ADA IKAFUTWA...! WALIPOFIKA DARASA LA NNE TU KURUDIA DARASA KUKAFUTWA...! KUIBUKIA FORM ONE MWAKA 2009 BAHATI IKAZIDI KUWAANGUKIA COZ KURUDIA FORM TWO KULIFUTWA....! KWA KUTHIBITISHA BAHATI YAO NA MATOKEO YAO YA MTIHANI WA FORM 4 YAMEFUTWA BAADA YA KUFELI SANA...! HIVYO YAMEPANGWA UPYA ILI WAWEZE KUFAULU...! DAH HAWA VIJANA WANA BAHATI...!

UHURU NA UMOJA…






UHURU NA UMOJA
(A).

Hapa pana picha mbili na zina maana tofauti lakini malengo pia ni tofauti jee kuna ukweli wowte na kama upo tufanye nini kuweza kuuzuia usi vurugike nikiwa na maana uhuru na umoja wetu watanzania picha ya kwanza ni ya mwaka 1960’ na yapili yake ni ya mwaka 2000’s

Hivi tunaona nini katika picha hizi mbili na tunajifunza nini?...picha ya kwanza ya mwaka 1960’s kuna watu wawili wa jinsia mbili tofauti nikiwa na maana mwanamke na mwanamume..wakiwa wameshika pembe za ndovu huu ni utajiri wa Tanzania unao lindwa kwa ngharama zozote na wananchi wa Tanzania…..yapili kuna ngao yenye alama ya mwenge unao mulika vitu vifuatavyo JEMBE NA SHOKA , BENDERA YA TANZANIA, NA MAWIMBI YA BAHARI kuonyesha utajiri wa baharini samaki nk. Pia kuna mlima wa Kilima njaro kuna utepe ulio shehenezwa maneno ya UHURU NA UMOJA…Ndio lengo sahihi la nembo hii.
(B).
 Hapa tunaona nembo ni ileile lakini maana tofaiti kwani ni mwaka 2000’s Yule Baka na Yule mama tulio waona katika miaka ile ya 1960’s wakiwa wame bebe meno ya Tembo na kila mmoja akiishia kusiko jilikana ule mwenge ulio kuwa uki mulika amani na upendo au Uhuru na umoja umeanza kuchoma nembo ile yale majembe na shoka hayako katika mpangilio yameanguka chini isitoshe ule utepo ulio kuwepo na uliokuwa umesheheni maneno matamu ya Uhuru na Umoja hayapo tene ….Labda kwa wakati huu yange andikwa CHUKUA CHAKO NA UAMBAE.
Sasa kama ni hivyo wazee wetu wale waliokuwa wakilinda ngao ili ya Uhuru na Umoja wakitokea na wakiwakuta ninyi MABINTI  NA  VIJANA (ambao kwasasa ni vitukuu vyao) Mkihamisha rasilimali hizo kwendanazo kusiko jurikana na wakataka kuwahoji nyinyi mtakuwa na lipi la kuji tetea au mta bung’aa kwa SONI?
“HIVYO WAKATI NI HUU WA KULINDA LASILI MALI ZA TAIFA KWA HESIMA YA WAASISI WA TAIFA HILI”

Friday, 14 June 2013

Mzanzibari mpinga utumwa




 Springfield Mzanzibari mpinga utumwa

 
ZANZIBAR



 


Leo tunamzungumzia Mzanzibari na Mwafrika wa kwanza, John Springfield ambaye aliishi Guilford, Uingereza baada ya kufanyakazi melini, kuendesha kampeni ya kuzuia utumwa, na hatimaye kuwa mwalimu wa kushona viatu katika Shule ya Robert Macdonald’s Guildford Mission Industrial School, nchini Uingereza.
Alizaliwa 1 Julai 1847, mtoto wa Chifu Jumbalowagee kule Zanzibar. Akiwa msituni akichuma matunda katika umri wa miaka tisa, alitekwa nyara na Wareno ambao baadaye waligundua kuwa alikuwa bado mdogo kwa umri kuingizwa utumwani.
Taarifa zinabainisha kwamba aliokolewa na mwanamke ingawa nyingine zinasema Dk Livingstone ndiye aliyemwokoa na kumtia kwenye ajira ya meli yake HMS Victoria. Ila asingeweza tena kurudi kwao kwa vile aliingizwa kwenye shughuli za utumwa na kula mkate (chakula cha Wazungu) na kusahau utamaduni wake.
Jina lake la asili halijulikani, lakini alipewa jina la John Springfield. Baada ya hapo akawa anafanyakazi kwenye meli hiyo ya HMS Victoria. Aliacha kazi na kwenda Amerika kuhubiri mapambano ya kuzuia biashara ya utumwa.
Kampeni yake dhidi ya utumwa kule Amerika haikupokelewa vizuri na akaamua kurudi tena Uingereza ambako mwaka 1870 alimuoa mama wa kizungu aliyeitwa Eliza Andrews ambaye alikuwa mtoto wa Williama Adrews aliyekuwa mtunza bustani.
John na Eliza walimzaa mtoto mmoja wa kike waliyemwita Miriam. John Springfield alifariki dunia Februari 21, mwaka 1891 na kuzikwa kwenye makaburi ya Stoughton Road, Guildford.
Miriam alizaa watoto wa kike wawili miaka ya 1896 na 1897 na mwaka 1899 alizaa mtoto wa kiume. Akiwa mjini Guildford, John Springfield alikuwa akifanyakazi ya kushona viatu, na kama nilivyosema hapo awali, alikuwa pia akifundisha ushonaji viatu. Huyu anakuwa Mzanzibari wa kwanza kuendesha kampeni dhidi ya utumwa na kule alikoishi.

Bajeti hiyooooooo!!!!!!2013/2014


Bajeti hiyooooooo...
2013/2014


WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa, amewasilisha bajeti ya serikali ya sh Trilioni 18.2 kwa mwaka wa fedha 2013/14 huku akiainisha vyanzo vipya vya mapato, kupunguza kodi na ushuru ili kuleta unafuu kwa wananchi.
Licha ya bajeti hiyo kutogusia kabisa suala la nyongeza ya mishahara ya watumishi wa umma, serikali imependekeza kupunguza kiwango cha kodi ya mapato ya ajira kutoka asilimia 14 hadi 13.
Akiwasilisha bajeti hiyo, iliyosomwa kwa saa 2.10, Mgimwa aliainisha vyanzo mbalimbali vitakavyoongeza mapato ya serikali lakini vingi vikiwa ni vilevile vya sigara, pombe, mafuta na magari wakati vyanzo vinavyohusu rasilimali za nchi kama madini, makampuni makubwa yakiendelea kuneemeka.
Waziri Mgimwa alisema kuwa ili kufikia malengo ya kiuchumi na mapato katika mwaka 2013/14 amependekeza kufanya maboresho ya sheria mbalimbali.
Sheria hizo ni pamoja na ile ya kodi ya ongezeko la thamani sura 148 akipendekeza kufuta msamaha wa VAT unaotolewa kwenye huduma za utalii, kutoa msamaha wa VAT kwa wazalishaji wa nguo nchini zinazozalishwa kwa pamba ya ndani kwa bidhaa na huduma.

“Kwa hatua hii mzalishaji wa nguo zinazotumia pamba ya hapa nchini hatalipa VAT kwenye manunuzi yake yote yanayohusiana na uzalishaji wa nguo hizo,” alisema.
Katika maboresho ya kodi ya mapato sura 332, Waziri Mgimwa alisema kuwa itaanzishwa kodi ya zuio ya asilimia 10 ya kamisheni ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya simu za mikononi.
Pia watoa huduma mbalimbali kama vile za ushauri wa kitaalamu na nyinginezo watatozwa kodi asilimia tano bila kujali kama kuna namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) au la.
Aliongeza kuwa itatozwa kodi ya zuio kwenye bidhaa zinazonunuliwa na serikali na taasisi zake kwa kiwango cha asilimia 2 huku msamaha wa kodi ya zuio kwenye ukodishaji ndege kwa walipa kodi wasio wakazi ukifutwa.
Mgimwa alifafanua kuwa katika sheria ya ushuru wa bidhaa sura 147 maboresho yatalenga kuongeza kiwango cha ushuru wa biashara kwenye magari yasiyo ya uzalishaji ya umri wa zaidi ya miaka 10 kutoka asilimia 20 hadi 25.
Pia kuanzisha kiwango kipya cha ushuru wa bidhaa cha asilimia tano kwenye magari ya uzalishaji yenye umri wa zaidi ya miaka 10. Kwamba lengo la maboresho ya sheria hiyo ni kupunguza uingiza wa magari chakavu, kulinda mazingira na kupunguza ajali.
Waziri alisema ameongeza ushuru kwa mafuta ya dizeli kutoka sh 215 hadi 217 kwa lita huku ushuru wa petroli ukipanda kutoka sh 339 hadi sh 400 kwa lita na mafuta ya taa ushuru unabaki vilevile wa sh 400.30 kwa lita.
Baadhi ya wataalumu wa uchumi waliotoa maoni yao jana, walisema kuongeza ushuru kwenye bei ya mafuta ya petroli na deseli kutasababisha mfumko wa bei, hivyo kuzidisha maumivu kwa wananchi.
Katika kulinda viwanda vya ndani bidhaa za kutoka nje kama mazuria, vipodozi, mafuta ya kujipaka, bunduki na risasi, boti za kifahari, ndege na helikopta zitatozwa ushuru kati ya asilimia 2.5 hadi 10.
“Kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 14.5 kwenye huduma zote za simu za kiganjani badala ya muda wa maongezi tu. Katika ushuru huu asilimia 2.5 zitatumika kugharamia elimu nchini,” alisema.
Katika mtiririko huo wa mapato, vinywaji baridi vimeongezeka kutoka sh 83 hadi 91 kwa lita, juisi ya matunda ya nchini kutoka sh 8 hadi 9, juisi ya matunda ya nje sh100 hadi 110, bia iliyotengenezwa kwa nafaka ya hapa nchini sh 300 hadi 341, bia zingine zote zimepanda kutoka ushuru wa sh 525 hadi 575 kwa lita.
Mvinyo wa zabibu za nchini utatozwa sh 160 kwa lita badala ya sh 145, mvinyo wa zabibu za nje ushuru umepanda kutoka sh 1,641 hadi 1,775 kwa lita, vinywaji vikali kutoka sh 2,392 hadi 2,631.
“Sigara zisizo na kichungi za nchini ushuru utapanda kutoka sh.8,210 hadi sh.9,031 kwa sigara elfu moja, sigara zenye kichungi za nchini zitapanda kutoka sh. 19,410 hadi 21,351 kwa siagara elfu moja,” alisema.
Kuhusu sheria ya usalama barabarani sura 168, marekebisho yatagusa kuongeza viwango vya ada ya mwaka ya leseni za magari ambapo gari lenye ujazo wa ijini 501.cc-1500.cc itapanda kutoka 100,000 hadi 150,000.
Mgimwa aliongeza kuwa gari lenye injini 1501.cc-2500.cc itapanda kutoka sh. 150,000 hadi 200,00 wakati gari la injini zaidi ya 2501.cc itapanda kutoka 200,000 hadi 250,000 huku injini chini ya 501cc ambayo ni ya "bodaboda na pikipiki haitatozwa kodi."