Saturday, 31 August 2013

.....BURIANI ASKOFU MOSES KULOLA WA ......(EAGT)

RAIS JAKAYA KIKWETE AMLILIA ASKOFU MOSES KULOLA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Moses Kulola ambaye ameafariki jana Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya AMI iliyoko Masaki mjini Dar Es Salaam akiwa na umri wa miaka 84.

Rais kikwete ameelezea mshtuko na huzuni yake katika Salamu za Rambirambi alizomtumia Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Bwana Brown Mwakipesile kufuatia kifo cha Askofu Mkuu Kulowa.  

“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za kifo cha Mtumishi wa Mungu wa muda mrefu na Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Marehemu Moses Kulola kutokana na maradhi yaliyomfanya wakati fulani apelekwe hadi India kupatiwa matibabu” amesema Rais Kikwete.

Rais Kikwete amesema alimfahamu Marehemu Askofu Moses Kulola kwa miaka mingi wakati wa enzi za uhai wake, kama Mtumishi Hodari wa Kiroho aliyejitoa vilivyo katika kuwahudumia Waumini wa Kanisa lake ambapo mahubiri yake yametoa mchango mkubwa katika kuimarisha imani za Waumini wake na kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kudumisha amani na utulivu wa nchi yetu. 

Aidha Rais Kikwete amesema kifo cha Askofu Mkuu, Moses Kulola kimeacha pengo kubwa siyo tu kwa Waumini wa Kanisa lake hapa nchini, bali pia miongoni mwa wapenda amani kote nchini na kwingineko duniani kwa vile enzi za uhai wake, Marehemu aliweza kufikisha ujumbe muhimu wa kiimani kupitia mahubiri yake kwa watu wa mataifa mbalimbali ndani na nje ya  Bara la Afrika.

“Kwa niaba yangu mwenyewe na Serikali ninayoingoza, ninakutumia wewe Katibu Mkuu wa Kanisa la Evangelical Assembies of God Tanzania, Bwana Brown Mwakipesile na Waumini wote wa Kanisa hilo Salamu za Rambirambi  kutoka dhati ya moyo wangu kwa kumpoteza Kiongozi muhimu wa Kiroho.  Ninawajulisha kuwa niko nanyi katika wakati huu mgumu kwa sababu msiba wenu ni msiba wetu pia. Sala na mioyo yetu iko nanyi wakati wa maombolezo ya kifo cha Kiongozi huyo shupavu wa dini. Nawaomba wote muwe wavumilivu na wenye subira kwani yote ni Mapenzi yake Mola”, amesema Rais Kikwete.

“Vilevile kupitia kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za Rambirambi na pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu, Askofu Mkuu, Moses Kulola kwa kumpoteza Baba, Kiongozi Shupavu na Mhimili wa familia.  Natambua fika kwamba hiki ni kipindi kigumu sana kwao cha maombolezo.  Natambua machungu yenu wakati huu na naungana nanyi katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke peponi roho ya Marehemu Moses Kulowa. Amina.”

Mazishi ya Marehemu, Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) yatafanyika mjini Mwanza Jumatano ijayo tarehe 4 Septemba, 2013.  Heshima za mwisho kwa mwili wa Kiongozi huyo zitatolewa siku ya Jumamosi tarehe 31 Agosti, 2013 katika Kanisa la EAGT karibu na Hospitali ya Temeke kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.    

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
29 Agosti, 2013

*** Na hapa dar24.com tunamwombea Askofu Moses Kulola apumumzike kwa amani. ******
 
 RAIS JAKAYA KIKWETE AMLILIA ASKOFU MOSES KULOLA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshtushwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Kiongozi wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Askofu Mkuu Moses Kulola ambaye ameafariki jana Agosti 29, 2013 katika Hospitali ya AMI iliyoko Masaki mjini Dar Es Salaam akiwa na umri wa miaka 84.

Rais kikwete ameelezea mshtuko na huzuni yake katika Salamu za Rambirambi alizomtumia Katibu Mkuu wa Kanisa hilo Bwana Brown Mwakipesile kufuatia kifo cha Askofu Mkuu Kulowa. ...Continue Reading
 
UMA WAMLILIA
ASKOFU MOSES KULOLA

Sunday, 25 August 2013

Kamati Kuu yamzuia Kagasheki kushiriki siasa mkoani Kagera

Tembo

Dodoma. Suala la kutimuliwa kwa madiwani wanane wa CCM katika Manispaa ya Bukoba limeingia sura mpya baada ya Kamati Kuu kuwazuia Meya, Dk Anatory Amani na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki kushiriki katika siasa mkoani humo hadi mwaka 2015.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya kubainika mgogoro wa viongozi hao, unakiumiza chama katika jimbo hilo.
Taarifa zilidai chanzo cha ugomvi kati ya Balozi Kagasheki na Dk Amani, ni kwa kila mmoja kutaka kugombea nafasi ya ubunge Jimbo la Bukoba mjini katika uchaguzi ujao. Na kwa uamuzi huo, Kagasheki na Dk Amani hawatashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Hata hivyo, akitangaza uamuzi huo jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema viongozi hao watakutana na Kamati Kuu leo na baada ya hapo utatangazwa uamuzi uliofikiwa.
Mbali na meya na mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, wengine walioitwa katika kikao hicho cha leo ni Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Costansia Buhinye, katibu wake, Averin Mushi pamoja na mwenyekiti wa chama Wilaya ya Bukoba, Yusuph Ngaiza na katibu wake, Janath Kayanda.
Kutokana na uamuzi huo, Kamati Kuu ambayo ilimaliza kikao chake saa 8:30 usiku wa kuamkia jana italazimika kukaa tena leo kuwaelezea uamuzi uliofikia.
Kumekuwapo na mgogoro mkubwa katika Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba, ukimuhusisha Kagasheki na baadhi ya madiwani kwa upande mmoja; na Dk Amani na kundi jingine la madiwani kwa upande mwingine.
Wakati wa mgogoro huo madiwani wamekuwa wakituhumiana ufisadi, na CCM imekwishawatuma viongozi wake wa juu kuingilia kati mgogoro huo akiwamo mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, lakini hakuna mafanikio yaliyopatikana.
Kufikishwa kwenye Kamati Kuu kwa suala hilo kumekuja baada ya uongozi wa CCM Mkoa wa Kagera kuamua kuwatimua uanachama madiwani hao, hatua ambayo ilikuwa inahatarisha nafasi zao na hivyo kukiingiza chama hicho kwenye uchaguzi mdogo.
Habari kutoka ndani ya vikao hivyo zinasema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa viongozi hao kuwajibishwa kwa kukiuka kanuni, kwa kuwa upo uamuzi wa chama unaokataza viongozi waliochaguliwa katika vyombo vya dola kuwajibishwa kwa staili hiyo.
Madiwani waliovuliwa uanachama na kata zao katika mabano ni pamoja na Richard Gaspar (Miembeni ), Murungi Kichwabuta (Viti Maalumu), Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe) na Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya (Kashai).
Wengine ni Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

chui

Albino waomba Serikali kuwapa elimu siyo misaada

Adhuhuri

Tanga. Chama cha Albino Mkoa wa Tanga (Tas), kimeomba Serikali
kuwatatulia kero zinazowakabili ikiwamo kuwezeshwa ili kujikimu na kuondokana na kutegemea misaada.
Akizungumza kwenye kongamano la kujadili changamoto zinazowakabili albino kuhusu afya na elimu, Katibu wa Tas Tanga, Innocent Haule, alisema Serikali haijawa tayari kuwasaidia.
Haule alisema jamii hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto ambazo Serikali imekuwa ikiwaahidi bila mafanikio na kwamba, inatakiwa kutekeleza ahadi zake.
Alitaja ahadi hizo kuwa ni kuwezeshwa kupata miradi yake, ambayo itasaidia kuondoa umaskini unaowakabili.
Awali, Mwenyekiti wa chama hicho, Nuru Shebula, aliwataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu wa ngozi kuwapeleka vituoni ili kutambuliwa. Alisema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwafungia ndani watoto wao, kuwanyika haki ya kupata elimu.
Mamba

Hoja ya Muungano inavyowavuta Watanzania katika mitandao ya kijamii

KWETU TANGA

MUUNGANO wa Bara na Visiwani umekuwa ukikumbwa na mfadhaiko mkubwa kutokana na baadhi yao kuuponda kwa sababu wanazojua wao.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
Katika mitandao ya kijamii watu wengi wamekuwa wakiujadili kila wanavyoweza. Handeni Kwetu Blog imeona ipost maoni ya Watanzania hao juu ya mkanganyiko huo wa Muungano kwa faida ya wote.
Maoni haya yamechukuliwa katika group linalojulikana kama Tanuru la Fikra, huku tukiamini kuwa tutafahamu japo kwa kiasi kidogo jinsi Muunganao huo unavyochukua nafasi ya kujadiliwa.
Hii ndio hoja iliyoingizwa na Abdul Hakeem
na kufuatiwa na maoni ya wengine hapo chini.
Hivi ikitokea TANZANIA ikaongozwa na rais mzanzibari.waziri mkuu mzanZibari.gavana mZanZibari.mabalozi karibu wote wa nje wawe wazanzibar.benki kuu iweko zbr .mji mkuu uwe zbr na mfano wa mambo hayo yaweko zbr. .jee WATANGANYIKA WATAENDELEA KUUPENDA MUUNGANO NA KUJIVUNIA UTANZANIA??
https://fbexternal-a.akamaihd.net/safe_image.php?d=AQApeiGpDHSxjf-c&url=https%3A%2F%2Ffbstatic-a.akamaihd.net%2Frsrc.php%2Fv2%2Fyo%2Fr%2FOKB7Z2hkREe.png

Omar Salim Shakur Shakur muungano haujaanza kukataliwa kwasababu etiya mafuta wazanbar wameanza kuukataa muunga tokea rais jumbe fisadi nyerere alipogundua akamfukuza abdul jumbe kwenye chama na kumueka chini ya ulinzi

Abdul Hakeem AMAN NGOSI zanzbr inanyimwa fursa za kujikwamua kiuchumi licha yakua na rasilimali nyingi na za kutosha kuwatumikia watu wake ambao ni milion moja.tuna bahari kubwa yakutosha.ni eneo zuri la biashara kwa AFRICA MASHARIKI /KUSINI.tuna ardhi nzuri ya kul...See More

Frank Mathias ha ha ha ha ha ha ha ha ha aiseee kweni zanzibar inaiongezea nn tanzania kuwa muungano ukivunjika itakuwa msala kivileee

Zarafi Rashidi faida ya muungano ipo unadhan wakiuvunja watanganyika wamezaa na wazbr na wengine wameweka makaz znbr tumien akil tujikomboe kiuchum hata watalii watatushangaa vikund vya wa2 wachache visitugombanishe

Omar Salim Shakur Shakur tatizo watanganyika asilimia kubwa ni waporipori hususan wanaochangia hii mada

Isaac Nyirenda Kanyunya Kwani Muungano ni chupa ya chai ambayo tumeishika wabara kwamba mnashindwa kutupokonya mkaivunja au!? FANYENI MAPINDUZI HUKOHUKO KWENU ANGUSHENI SERIKALI MUWEKENI PONDA HAPO JUU FULLSTOP. Au kaeni chini ongeeni na rais wenu ateuwe mawaziri wake mjenge wizara zote, mteue mkuu wa majeshi na polisi pia na mambo kama hayo then MKOMESHENI ASIJE BARA MBAKI HUKO HUKO. Muone kama sisi TUTALALAMIKA AU KUANZA VITA!

Peter Mwambola Mi mwenyewe MUUNGANO siutaki kabisa basi tu sina la kufanya tu naongea toka moyoni kabisa

Mathewricky Don Yungweogenesis Sawa baba yetu wa taifa ni fisadi ila wa kwenu mtatawaliwa mpaka na vitukuu na vilembwe vyake vyote pumbafu ninyi. Si mkae kimya msije huku fungeni mipaka wa huko wa huko wa huku wa huku sio mikeleleee tatzo lenu wengi wenu hamjitambui matokeo yake wac...See More

Omar Salim Shakur Shakur tatizo watanganyika asilimia kubwa ni waporipori hususan wanaochangia hii mada

Marryape la Uniquebabe Kua na wafanyakazi wa kibongo n kosa la nani????? Nyie bwana mbona wazenji kibao mnasoma kwe vyuo vyetu na ndo jambo la mcng lkn hakuna anaewafukuza wala kuhoji???bhana eeehhh km vp fanyeni yenu mctupigie kelele

Abdul Hakeem kama tanganyk hainufaiki na muungan kwanni NYERERE alikataa serikali tatu?na kwanini watanganyika ndio wanaoupenda muungano?

Frank Mathias we jamaa haujielewi aisee @omary

Omar Salim Shakur Shakur isaac unaongea usilolijua tunasubirikura ya maoni fullstop

Magdalena Ngonyani yes marryape, wao wamejaa sana huku bara sisi hatusemi, vyuo vyote wamevijaza na asilimia za bodi ya mikopo wanachukua kubwaa, mfano mzuri chuo cha UDOM masters wamejaa wazenji tu robo tatu nzima

Isaac Nyirenda Kanyunya We Abdul hayo mafuta yako wapi tusiotaka kuwaachia!!?? Hiyo 80% ya wafanyakazi inatoka bara kwakuwa wapemba wote hawajasoma hawawezi kuongea na watalii wao wamekimbilia Bara huku kuja kufungu Magenge na maduka sasa cha ajabu nini hapo!!!??
 
Punda milia wa Tanzania
 
Kesi ya kufutwa Muungano yatajwa Z’bar

MBUGA ZA WANYAMA

Kesi ya kufutwa Muungano

 yatajwa Z’bar

Zanzibar. Kesi ya aina yake ya kikatiba inayotaka Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika ufutwe imetajwa Mahakama Kuu Zanzibar huku wadai wakieleza kuwa kesi yao inacheleweshwa.
Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi kwa vile anayepaswa kuisikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu hakuwepo mahakamani.
Wakili wa watu 1,950 wa Unguja na Pemba waliofungua kesi hiyo, Philip Ojode wa Mombasa Kenya alidai kuwa miezi minne sasa imepita tangu kesi hiyo kufunguliwa mahakamani lakini haijasikilizwa.
Alimtaka Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar kuto amri kwa wadaiwa katika kesi hiyo ambao miongoni mwao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwa kuwapa siku saba kujibu maelezo ya kesi hiyo.
Wakili wa Serikali, Mark Mulwambo anayesaidiwa na Fatma Salehe alidai kuwa Mrajis wa Mahakama Kuu hana mamlaka ya kutoa amri yoyote katika kesi hiyo.
Mrajis Kazi alisema kuwa ni kweli yeye hana mamlaka ya kutoa amri yoyote kuhusiana na kesi kwa vile mamlaka hayo yako kwa majaji wa Mahakama Kuu na hivyo hawezi kutoa uamuzi.
Mrajisi wa Mahakama Kuu aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 13,2013 kwa kusikilizwa na Jaji Mkuu ambaye ilielezwa jana kuwa alipata safari ya ghafla ya kwenda Dar es Salam.
Mara ya mwisho ilipotajwa kesi hiyo Julai 25 mwaka huu mbele ya Mrajis wa Mahakama Kuu, Jaji Mkuu alikuwa safarini Kagera kushiriki sherehe za kitaifa za siku ya mashujaa.

KWETU TANGA