Taarifa |
Rwanda |
SADC |
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imetoa onyo kali kwa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kwa kumtaka aachane mara moja na na fikra zozote mbaya alizonazo ikiwamo mipango yake ya kuihujuma Serikali ya Tanzania na watu wake.
Onyo hili limefuatia nchi wanachama wa SADC kufuatilia kwa makini mzozo wa kidiplomasia ambao Kagame aeuiubua na amekuwa anaukuza hadharani na kichinichini dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na Tanzania kwa ujumla.
Habari hizi zimetolewa na viongozi wa juu wa SADC na maofisa wa Serikali, waliokuwa katika ujumbe wa Rais Jakaya Kikwete alipokwenda kuhudhuria Mkutano wa viongozi wa Maziwa Makuu huko Uganda hivi karibuni. Aidha, imethibitishwa kuwa tayari Jumuiya hiyo imekwisha mpatia ujumbe huo mmoja wa mawaziri aliyekuwa ameandamana na Kagame muda mfupi baada ya kikao chake na Kikwete.
Kiongozi mmoja wa juu wa Msumbiji ambaye alikuwa pia Uganda, alikaririwa akimueleza Waziri aliyeandamana na Kagame kuwa “Nchi za SADC zinafahamu kuwa Rais Kagame hajafurahishwa na uamuzi wa Tanzania wa kupeleka vikosi vyake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Hata hivyo Kagame anapaswa kuelewa kuwa ilichofanya Tanzania ulikuwa ni msimamo wa pamoja wa nchi za SADC."
Aidha Kiongozi huyo aliendelea kusema "hivyo basi vitisho au uvamizi wa kijeshi dhidi ya Tanzania utachukuliwa ni uvamizi dhidi ya SADC, na tutakuwa tayari kuingia vitani kupigana upande wa Tanzania.”