MSHAMBULIAJI hatari wa timu ya
Mashorobaro iliyopo kijiji cha Komsala, wilayani Handeni, mkoani Tanga, Malilo
Gerevas, amesema kwamba wataendelea kuwanyanyasa watani wao wa jadi, Men Stone
kwa kuwafunga kila wanapokutana uwanjani.
Timu zote mbili zinapatikana
katika kijiji hicho kinachotajwa kuwa na msisimko wa aina yake katika mpira wa
miguu kiasi cha kuleta raha kwa wadau wa michezo maeneo hayo.
Akizungumza na Handeni Kwetu
Blog kijijini kwao juzi, Gerevas alisema kwamba wao wana timu nzuri na
iliyosheheni vijana wadogo, jambo linalowafanya wawe na kasi uwanjani.
“Wale ni ndugu zetu lakini
katika masuala ya soka wataendelea kulia kila siku kwakuwa lazima tuwafunge ili
waone namna gani sisi ni bora kuliko wao tunapokuwa dimbani".
“Sisi wote zamani tulikuwa timu
moja ya Men Stone, ila tukaona hamu ya kuanzisha timu nyingine na kuitwa
Masharobaro na kufanikiwa kuonyesha shauku yetu michezoni,”
alisema Gerevas.
Licha ya kuwa na shauku kubwa
ya kuendeleza vipaji vyao, ila Gerevas ni miongoni mwa vijana wengi wanaoshindwa
kuonyesha cheche zao kutokana na ukosefu wa mipango ya kukuza soka la vijana
katika wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.
Kwetu Tanga |
No comments:
Post a Comment