Friday, 2 August 2013

'Uchaguzi umekumbwa na kasoro kubwa




chaguzi wa Rais nchini Zimbabwe ulikuwa ‘kichekesho kikubwa,’ Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai amesema, akituhumu udanganyifu wa kura uliofanywa na kambi ya mpinzani wake Rais Robert Mugabe.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Tsvangirai alisema uupigaji kura wa Jumatano ulikuwa ‘upuuzi na si halali’.
Kundi kubwa la waangalizi mapema lilisema kufikia hadi watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.
Chama cha Bw Mugabe ambacho kinadai kushinda, kimekanusha tuhuma hizo kikisema upigaji kura ulikuwa shwari.
Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Afrika, Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, alisemsa kwenye tathimini yao ya awali kuwa upigaji kura ulikuwa huru na haki.
Makundi mengine ya waangalizi yalisifia hali ya amani katika uchaguzi huo.
Kuhesabu kura ulianza kulianza usiku na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC) ina siku tano za kutangaza nani mshindi katika uchaguzi huo.
Tayari polisi wameonya kuwa watachukua hatua dhidi ya yeyote atakayejaribu kuvujisha habari za matokeo. Ni kinyume cha sheria kutangaza matokeo yasiyo rasmi.
Vikosi vya ziada baadhi vikiwa na vifaa vya kupambana na waandamanaji tayari viko mjini Harare.
Hatua za kisheria huenda zikafuata sasa, kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Andrew Harding akiripoti kutoka Johannesburg.
Lakini megi yatategemea iwapo majirani wa Zimbabwe watapitisha uchaguzi huo, mwandishi wa BBC anaongezi.

Akizungumza kwenye makao makuu ya chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) mjini Harare, Bw Tsvangirai alisema: "Hitimisho letu ni kuwa uchaguzi huu ni kichekesho kikubwa.’

"Uhalali wa uchgauzi huu umeharibiwa na ukiukwaji wa sheria na shughuli za kiutawala ambazo zimeathiri matokeo yake.”
"Ni utani ambao hauonyeshi matakwa ya watu."
Bw Tsvangirai alizungumza muda mfupi baada ya mtandao wa waangalizi (Zimbabwe Election Support Network-ZESN) kusema kuwa uchaguzi huo ‘umekumbwa na kasoro kubwa".
Katika taarifa yake rasmi ZESN limesema wapiga kura muhimu kufikia asilimia 82 walizuiwa katika vituo vya kupigia kura maeneo ya mijini ambako ni ngome ya Bw Tsvangirai.
Katika maeneo ya vijijini am, ambako ni ngome ya Rais Mugabe ni asilimia 38, kundi hilo limeongeza.
Jumatano wanavijiji, mawakala wa MDC kwenye vituo vya kupigia kura na ZESN walisema kumekuwa na kasoro kadhaa katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Masvingo.
Walisema viongozi wa jadi na wakuu wa vijiji waliwapanga watu kwenye mistari na kuwalazimisha kutembea kuelekea vituo vya kupigia kura na kuwapa namba za kupigia kura kama vile kuwahakiki wamempigia kura nani.
Wanatuhumu kuwa kwenye maeneo haya baadhi ya watu wasomi walilazimishwa kujifanya hawajui kusoma na kuandika na wakasaidiwa kupiga kura ambazo zilikuwa ni kwa Zanu-PF.
Msemaji wa Zanu-PF Mtaalam wa Saikolojia Maziwisa alikanusha kuwa wapiga kura wengi wamezuiwa makusudi kujiandikisha.
Amekiri kuwa kulikuwa na kasoro kadhaa lakini akafafanua kuwa vyama vyote vimeathirika.
"Ni muhimu kumbuka kuwa hiyo kwa sehemu ilisababishwa na ukweli kuwa baadhi ya vifaa muhimu Waziri wa Fedha Tendai Biti, anayetoka chama cha MDC alikuwa," Bw Maziwisa aliiambia BBC.
"Ukiaangalia hali ya Zimbabwe utakuwa na hitimisho moja tu. Na hii ni juu ya zaidi ya miaka mine iliyopita tumefanya jitihada za kutosha kufanya mazingira ya Zimbabwe yawe mazuri inavyowezekana ili uchaguzi uwe huru na hali.."

Rais Jakaya Kikwete

Marais wakosa mkutano




Dar es Salaam. Mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukifanyika Nairobi, Kenya, umemalizika jana bila kuwepo kwa
Rais Jakaya Kikwete, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hata hivyo, Rais Kikwete aliwakilishwa na Makamu wake, Dk Mohammed Gharib Bilal, huku Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikisema Rais Kikwete alishindwa kuhudhuria mkutano huo kwa sababu alikuwa na ugeni wa Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra.
Kukosekana kwa viongozi hao katika mkutano huo kumetafsiriwa kuwa kunatokana na mvutano uliopo sasa kuhusu majeshi ya vikosi vya kulinda amani na waasi wa kikundi cha M23 wanaoipinga Serikali ya Congo.
Waasi hao wanadaiwa kuungwa mkono na Serikali ya Rwanda.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema, “Rais alikuwa na ugeni wa Waziri Mkuu wa Thailand ndiyo maana hakuweza kuhudhuria ila alikuwepo Makamu wa Rais. Hilo la viongozi wa Rwanda na DRC kutokuwepo siwezi kulisemea chochote.”
Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi za Maziwa Makuu, walitoa taarifa zao na kujadiliwa.

Wednesday, 31 July 2013

SIKU YA MAAMUZI ZIMBABWE




Foleni ya Wapiga kura
Raia wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais unaotajwa kuwa na ushindani mkali huku kukiwa na madai ya udanganyifu. Rais Robert Mugabe wa Zanu-PF anachuana na Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai wa MDC.

Wasiwasi kuhusu uchaguzi Zimbabwe



UCHAGUZI ZIMBABWE...2013

 

 

Wasiwasi kuhusu uchaguzi 

Zimbabwe

 




Mugabe anamenyana na Morgan Tsvangirai kwenye uchaguzi mkuu
Mkuu wa waangalizi wa uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kanda ya Afrika Kusini, Bernard Membe, ameelezea wasiwasi mkubwa kuwa daftari la wapiga kura lingali kutolewa siku moja kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika nchini humo.
Hii ni licha ya kuwa daftari hilo kuwa kiungo muhimu kwenye uchaguzi utakaofanyika Jumatano.
Chama cha MDC chake hasimu wa rais Mugabe, Morgan Tsvangirai, kimesema kinajiandaa kwenda mahakamani kuweza kupata daftari hilo.
Shughuli ya kupiga kura itamaliza serikali ya Muungano kati ya MDC na chama cha rais Mugabe Zanu-PF .
Rais Mugabe anataka kugombea urais hata baada ya kuitawala nchi hiyo kwa miaka 33. Anamenyana na waziri mkuu Morgan Tsvangirai
Ikiwa imesalia siku moja kabla ya upigaji kura, hakuna chama kilichopokea sajili la wapiga kura.
Mahasimu hao wawili wakuu, wamekuwa wakigawana mamlaka tangu mwaka 2009, baada ya mkataba kuafikiwa kwa usaidizi wa muungano wa nchi za ukanda wa Afrika Kusini SADC, ili kumaliza mgogoro wa kisiasa uliosababisha vurugu za baada ya uchaguzi 2008.
Bwana Membe, ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Tanzania alisema kuwa daftari la wapiga kura sio siri kubwa na kuwa lilipaswa kutolewa zamani sana.
"lazima itolewe kwa wapiga kura ili waweze kuhakiki majina yao, waweze kujua watakapopiga kura,'' alisema bwana Membe.
Katibu mkuu wa chama cha MDC Tendai Biti alisema kuwa chama hicho kitachukua hatua za kisheria dhidi ya tume ya uchaguzi ili kuweza kupata sajili hilo.


KWA NINI MAOFISA USALAMA WANAUAWA?


 
 
 
 
 
 
 
Damu zikimtoka marehemu baada ya kupigwa risasi.

 

KWA NINI MAOFISA USALAMA WANAUAWA? 

 

 


Haruni Sanchawa na Makongoro Oging'

WANANCHI wengi walioshuhudia Afisa Usalama wa Taifa  akiuawa Tegeta Kibaoni jijini Dar Ijumaa iliyopita, waliuliza kwa nini maofisa  wa idara hiyo siku hizi wamekuwa wakiuawa kirahisi?

Mwili wa Ramadhani Mrutu ukiwa umefunikwa.
Hakukuwa mwenye jibu sahihi na badala yake wakawa wanaikodolea macho maiti ya afisa huyo aliyetambulika kwa majina ya  Ramadhani Mrutu ambaye alikuwa amepigwa risasi mchana kweupe na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi maeneo hayo ya Tegeta kibaoni.
 
Mwili ukitolewa eneo la tukio.
Wananchi hao walikuwa wakirejea kifo kingine chenye utata cha Afisa Usalama wa Taifa, Peter Tyenyi ambaye maiti yake ilikutwa kisimani karibu na ofisi zao zilizopo Kijitonyama jijini Dar Mei 27, mwaka huu. Hadi leo hakuna chombo chochote cha dola kilichotoa taarifa kuelezea kilichomuua afisa huyo.
Damu ikiwa imetapakaa.
Waandishi wetu waliokwenda Tegeta Kibaoni mara tu baada ya kupata habari za kuuawa kwa afisa Mrutu, waliambiwa na mashuhuda kuwa alipofika kwenye gereji moja ambayo huwa anaitumia kutengeneza gari lake alivamiwa na mtu mmoja aliyekuwa na bastola.
“Yule jambazi alimnyang’anya mkoba aliokuwanao kisha kumpiga risasi tatu, wengi tulishituka sana tuliposikia milio ya bunduki,” alisema shuhuda aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari.
 Chanzo chetu cha habari kilisema kuwa ofisa huyo alikuwa ametokea benki kuchukua fedha ambazo kiasi chake hakikufahamika mara moja na alipotoka hapo alienda moja kwa moja katika gereji ambayo mauaji yalifanyika.
 “Inaonekana mtu aliyemuua akiwa na dereva wa pikikipi walitoka naye mbali hadi kufika naye pale gereji na kufanya unyang’anyi na mauji hayo,” kilisema chanzo hicho.
 
Gari lenye mwili wa marehemu likiondoka eneo la tukio.
Kikaongeza Mrutu alipigwa risasi saa 6.15 mchana, risasi ya kwanza ilimpata mguuni, ya pili kiunoni, ya tatu kifuani hali iliyosababisha kifo chake palepale.
Kiliendelea kutiririkia kuwa, baada ya unyama huo majambazi hayo yaliondoka na begi dogo alilokuwa nalo na kutokomea kusikojulikana.
 
 
 
 
 
 
 
 
Wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP  Camilius Wambura aliliambia gazeti hili kuwa upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea.
“Tunafanya upelelezi ili tuweze kuwatia mbaroni wahusika,” alisema Kamanda Wambura alipopigiwa simu na gazeti hili.Chanzo:www.globalpublishers.info