Damu zikimtoka marehemu baada ya kupigwa risasi.
KWA NINI MAOFISA USALAMA WANAUAWA?
Haruni Sanchawa na Makongoro Oging'
WANANCHI wengi walioshuhudia Afisa Usalama wa Taifa akiuawa Tegeta Kibaoni jijini Dar Ijumaa iliyopita, waliuliza kwa nini maofisa wa idara hiyo siku hizi wamekuwa wakiuawa kirahisi?
Hakukuwa mwenye jibu sahihi na badala yake wakawa wanaikodolea macho maiti ya afisa huyo aliyetambulika kwa majina ya Ramadhani Mrutu ambaye alikuwa amepigwa risasi mchana kweupe na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi maeneo hayo ya Tegeta kibaoni.
Mwili ukitolewa eneo la tukio.
Wananchi hao walikuwa wakirejea kifo kingine chenye utata cha Afisa
Usalama wa Taifa, Peter Tyenyi ambaye maiti yake ilikutwa kisimani
karibu na ofisi zao zilizopo Kijitonyama jijini Dar Mei 27, mwaka huu.
Hadi leo hakuna chombo chochote cha dola kilichotoa taarifa kuelezea
kilichomuua afisa huyo.Waandishi wetu waliokwenda Tegeta Kibaoni mara tu baada ya kupata habari za kuuawa kwa afisa Mrutu, waliambiwa na mashuhuda kuwa alipofika kwenye gereji moja ambayo huwa anaitumia kutengeneza gari lake alivamiwa na mtu mmoja aliyekuwa na bastola.
“Yule jambazi alimnyang’anya mkoba aliokuwanao kisha kumpiga risasi tatu, wengi tulishituka sana tuliposikia milio ya bunduki,” alisema shuhuda aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Chanzo chetu cha habari kilisema kuwa ofisa huyo alikuwa ametokea benki kuchukua fedha ambazo kiasi chake hakikufahamika mara moja na alipotoka hapo alienda moja kwa moja katika gereji ambayo mauaji yalifanyika.
“Inaonekana mtu aliyemuua akiwa na dereva wa pikikipi walitoka naye mbali hadi kufika naye pale gereji na kufanya unyang’anyi na mauji hayo,” kilisema chanzo hicho.
Gari lenye mwili wa marehemu likiondoka eneo la tukio.
Kikaongeza Mrutu alipigwa risasi saa 6.15 mchana, risasi ya kwanza
ilimpata mguuni, ya pili kiunoni, ya tatu kifuani hali iliyosababisha
kifo chake palepale.Kiliendelea kutiririkia kuwa, baada ya unyama huo majambazi hayo yaliondoka na begi dogo alilokuwa nalo na kutokomea kusikojulikana.
Wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura
aliliambia gazeti hili kuwa upelelezi juu ya tukio hilo unaendelea.“Tunafanya upelelezi ili tuweze kuwatia mbaroni wahusika,” alisema Kamanda Wambura alipopigiwa simu na gazeti hili.Chanzo:www.globalpublishers.info
No comments:
Post a Comment