Marais wakosa mkutano |
Dar es Salaam. Mkutano wa wakuu wa nchi za Maziwa Makuu uliokuwa ukifanyika Nairobi, Kenya, umemalizika jana bila kuwepo kwa
Rais Jakaya Kikwete, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hata hivyo, Rais Kikwete aliwakilishwa na Makamu
wake, Dk Mohammed Gharib Bilal, huku Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa ikisema Rais Kikwete alishindwa kuhudhuria
mkutano huo kwa sababu alikuwa na ugeni wa Waziri Mkuu wa Thailand,
Yingluck Shinawatra.
Kukosekana kwa viongozi hao katika mkutano huo
kumetafsiriwa kuwa kunatokana na mvutano uliopo sasa kuhusu majeshi ya
vikosi vya kulinda amani na waasi wa kikundi cha M23 wanaoipinga
Serikali ya Congo.
Waasi hao wanadaiwa kuungwa mkono na Serikali ya Rwanda.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema, “Rais alikuwa na ugeni wa Waziri
Mkuu wa Thailand ndiyo maana hakuweza kuhudhuria ila alikuwepo Makamu wa
Rais. Hilo la viongozi wa Rwanda na DRC kutokuwepo siwezi kulisemea
chochote.”
Mawaziri wa ulinzi kutoka nchi za Maziwa Makuu, walitoa taarifa zao na kujadiliwa.
No comments:
Post a Comment