|
Swala |
|
Twiga |
|
Simba |
Pangani. Hifadhi ya Taifa Tanapa, imewataka wananchi waishio
karibu na
hifadhi za wanyamapori nchini, kubadilika na kuacha tabia ya
kuishi kimazoea badala yake wawe wabunifu kwa kupanda mazao ambayo
hayashambuliwi na wanyama waishio katika maeneo ya mbuga za wanyama.
Meneja Ujirani Mwema Taifa, Ahmed Mbugi alisema
endapo wakazi wa maeneo jirani watapanda mazao kama ufuta, pilipili za
kuwasha pamoja na miti ya kutanda itasaidia kuzuia njia za wanyama
kupita kwenye maeneo yao.
Hayo aliyasema wakati wa mafunzo ya uandishi wa
masuala ya hifadhi yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za
Vijijini na Mazingira na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wilayani
Pangani hivi karibuni.
|
Tanga Kwetu |
No comments:
Post a Comment