MBUGA ZA WANYAMA |
Kesi ya kufutwa Muungano
yatajwa Z’bar
Zanzibar. Kesi ya aina yake ya kikatiba inayotaka Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika ufutwe imetajwa Mahakama Kuu Zanzibar huku wadai wakieleza kuwa kesi yao inacheleweshwa.
Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Mrajis wa Mahakama Kuu
ya Zanzibar, George Kazi kwa vile anayepaswa kuisikiliza Jaji Mkuu wa
Zanzibar, Omar Othman Makungu hakuwepo mahakamani.
Wakili wa watu 1,950 wa Unguja na Pemba
waliofungua kesi hiyo, Philip Ojode wa Mombasa Kenya alidai kuwa miezi
minne sasa imepita tangu kesi hiyo kufunguliwa mahakamani lakini
haijasikilizwa.
Alimtaka Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar kuto amri
kwa wadaiwa katika kesi hiyo ambao miongoni mwao ni Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar kwa kuwapa siku saba kujibu maelezo ya kesi hiyo.
Wakili wa Serikali, Mark Mulwambo anayesaidiwa na
Fatma Salehe alidai kuwa Mrajis wa Mahakama Kuu hana mamlaka ya kutoa
amri yoyote katika kesi hiyo.
Mrajis Kazi alisema kuwa ni kweli yeye hana
mamlaka ya kutoa amri yoyote kuhusiana na kesi kwa vile mamlaka hayo
yako kwa majaji wa Mahakama Kuu na hivyo hawezi kutoa uamuzi.
Mrajisi wa Mahakama Kuu aliahirisha kesi hiyo hadi
Septemba 13,2013 kwa kusikilizwa na Jaji Mkuu ambaye ilielezwa jana
kuwa alipata safari ya ghafla ya kwenda Dar es Salam.
Mara ya mwisho ilipotajwa kesi hiyo Julai 25 mwaka
huu mbele ya Mrajis wa Mahakama Kuu, Jaji Mkuu alikuwa safarini Kagera
kushiriki sherehe za kitaifa za siku ya mashujaa.
No comments:
Post a Comment