Sunday, 25 August 2013

Albino waomba Serikali kuwapa elimu siyo misaada





Adhuhuri




Tanga. Chama cha Albino Mkoa wa Tanga (Tas), kimeomba Serikali
kuwatatulia kero zinazowakabili ikiwamo kuwezeshwa ili kujikimu na kuondokana na kutegemea misaada.
Akizungumza kwenye kongamano la kujadili changamoto zinazowakabili albino kuhusu afya na elimu, Katibu wa Tas Tanga, Innocent Haule, alisema Serikali haijawa tayari kuwasaidia.
Haule alisema jamii hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto ambazo Serikali imekuwa ikiwaahidi bila mafanikio na kwamba, inatakiwa kutekeleza ahadi zake.
Alitaja ahadi hizo kuwa ni kuwezeshwa kupata miradi yake, ambayo itasaidia kuondoa umaskini unaowakabili.
Awali, Mwenyekiti wa chama hicho, Nuru Shebula, aliwataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu wa ngozi kuwapeleka vituoni ili kutambuliwa. Alisema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwafungia ndani watoto wao, kuwanyika haki ya kupata elimu.
Mamba

No comments:

Post a Comment