Kinana …..”Msigwa kortini”
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Abdul-rahman Kinana amemfungulia kesi Mbunge wa Iringa Mjini, Peter
Msigwa (Chadema), kutokana na kumtuhumu anajihusisha na ujangili na biashara
haramu ya pembe za ndovu.
Kinana amefungua kesi hiyo katika
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na kitendo cha Mbunge huyo kutoa
tuhuma hizo dhidi yake kwa nyakati tofauti nje na ndani ya Bunge, pia alikataa
kuzikanusha na kumuomba radhi.
Inadaiwa kuwa Aprili 21 mwaka huu
Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa tuhuma hizo kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Mbuguni wilayani
Nyamagana mkoani Mwanza.
Aidha
alizitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Kambi ya Upinzani katika
Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/2014. Katika
hati ya madai, Kinana anadai kuwa kutokana na tuhuma hizo ameharibiwa tabia
yake, uaminifu, hadhi yake kitaaluma na weledi na kumfanya achukiwe na
kudharauliwa katika jamii.
Anadai jina lake na heshima ambayo ameijenga kwa muda mrefu, vimeharibiwa na Msigwa kwa nia mbaya, pia kwa tuhuma hizo anazosisitiza kuwa ni za uwongo, licha ya kumsababishia maumivu ya kisaikolojia, pia zimemsababishia hasara ya fedha.

Anadai kuwa kabla ya tuhuma hizo alikuwa
katika hatua za mwisho za mchakato wa mazungumzo ya mradi wa ubia wa kilimo cha
mboga na mwekezaji kutoka kampuni ya nje, lakini tuhuma hizo zimesababisha
kampuni hiyo kuvunja majadiliano hayo.
Kinana anadai kuwa sababu
iliyotolewa na kampuni hiyo kuvunja mazungumzo hayo ni kutajwa kwake na mbunge
huyo kuwa ni jangili anayejishughulisha na biashara hiyo.
Kwa mujibu wa hati ya madai, Mradi
huo ulikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni nne, Hisa za ushiriki wa
Kinana zilikuwa ni asilimia 25 katika kipindi cha miaka mitano hivyo
anatathmini kuwa amepata hasara ya Sh milioni 350.
Kinana anaiomba Mahakama hiyo
imwamuru Msigwa amlipe fidia ya Sh milioni 350 kama hasara rasmi, pamoja na
fidia ya maudhi na fidia ya hasara ikiwemo gharama za kesi.
Aidha anaiomba Mahakama imwamuru
amlipe riba kwa kiwango kitakachopangwa na Mahakama, tangu tarehe ya hukumu
hadi malipo ya mwisho, imwamuru kufuta tuhuma dhidi yake na kumuomba radhi kwa
kuchapisha katika magazeti mawili ya Kingereza na mawili ya Kiswahili
yanayosambazwa nchini.
Pia Mahakama itoe zuio la kudumu kumzuia Msigwa, au wakala wake kutoa au kuchapisha taarifa zozote za kashfa dhidi yake. Katika hati ya madai amenukuu baadhi ya kauli za Msigwa, ikiwemo “Kinana (naomba waandishi wa habari mnisikie na nyie Usalama wa Taifa mkapeleke habari) hana sifa za kupita barabarani na kuwaambia Watanzania waiamini CCM. Kinana mikono yake si misafi.”

“Hata
kwenye Nassaco, Shirika la Meli Tanzania kuna harufu ya ufisadi ndani yake;
ajibu hoja…Kinana meli zake ndizo zinazohusika kubeba pembe za ndovu nchini.
hajajibu hoja hizo! Kwa siku nchi hii tembo 67 wanauawa. Hao ndio
wanaokifadhili Chama Cha Mapinduzi, halafu wanakuja eti kuwashawishi Watanzania
muwasikilize na kwamba Chama Cha Mapinduzi eti ni kizuri.”
“.Haya mambo ninayoongea ni hatari kwa sababu haya yote ni
majangili ni organized Crime. Ni mtandao wa Kimafia, uko duniani kote, unaweza
ukatuua lakini wabunge tumesimama tunawatetea…”
No comments:
Post a Comment