KAGAME CUP
WAZIRI wangu wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, katu usikubali kudanganywa juu ya
ushiriki wa timu zetu kwenye michuano ya Kagame Cup huko nchini Sudan.
Hakuna amani kamwe. Ndio maana majeshi ya kulinda amani yapo huko na upinzani mkubwa wanakutana nao, sasa kwanini Membe ajitowe mhanga kama Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa? Nahisi kuna mchezo mchafu unataka kufanywa juu ya Taifa hili, hasa wanasiasa katika kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2015....
“Ingawa Nicholas Musonye, Katibu wa CECAFA anang'ang'ania, akikutaka usiingilie, lakini kesho madhara yakitokea, kwa timu zetu za Simba, Yanga na Falcom moja wapo kupigwa bomu na wachezaji kadhaa kufa, hakika mengi yataelekezwa kwako”.
Si ajabu hata siasa zitaibuliwa juu ya utendaji wako wa kazi.
Na hizi mbio za Urais ndio kabisa. Kila baya litaelekezwa kwako.
Kumbuka, leo watu wanahoji uhalali wa Edward Lowassa juu ya Kashfa ya Richmond. Ingawa yeye anasema ni uamuzi wa pamoja wa serikali, lakini bado yeye anapewa lawama kwakuwa alikuwa Waziri Mkuu.
Naheshimu sana michezo, na kuipenda hii michuano, lakini kwanini ziende wakati hakuna amani? Musonye anasema kuzifungia timu zitakazogomea mashindano hayo, kwanini asianze kwanza na timu yake ya Tusker iliyojitoa kwenye mashindano hayo?
Tusker ni ya Kenya na yeye anatokea Kenya, kwanini asianze kwanza nchini kwao? Hakika, huwa simpendi Musonye kwasababu anapenda maslahi yake binafsi kuliko utu.
Hivyo basi, kama mashindano haya yana maslahi kwake, achukuwe timu za Kenya na azipeleke huko. Madamu Tanzania inaongozwa kwa utawala wa sheria na kuelewana pia, basi hili la amani ya Sudan na timu zetu lazima liangaliwe upya.
Hakika, Ukidanganyika tu, timu ziende, kuna watu wanaweza kufanya hujuma kwa makusudi ili kukitia dosari katika utendaji wako. Nasema haya kama mdau wa michezo, kama Mtanzania na ninayeheshimu pia utendaji wa viongozi wangu.
Katika hili la Kombe la Kagame, Membe shikilia msimamo wa Amani hakuna Sudan na Simba, Yanga, Falcome zisiendem na kama ziking'ang'ania kwenda kitakachowatokea, basi kiwe kwa faida yao na hasara yao pia. Tukae chini, tujitafari, tujiangalie vizuri na hasa hawa wenye uwezo wa kusema na kesho pia wataulizwa maswali ikitokea tofuati…..(lakini lazima tukumbuke michezo ni kioo cha amani na wanamichezo ni mabarozi wanchi husika pia kati ya mataifa husika)
Mungu ibari Tanzania.....

No comments:
Post a Comment