SHEIKH
PONDA NI MCHOCHEZI?????
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, amesema Katibu
Mkuu wa Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda ni mchochezi sugu
mwenye nia ya kumwaga sumu ili kuvuruga misingi ya amani na utulivu
nchini.
Balozi Seif alitoa kauli hiyo juzi baada ya kupata
futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya UVCCM katika ukumbi wa Gymkhana,
kisiwani Unguja.
Alisema dhifa
za mashirikiano na udugu hufanyika kwenye nchi zilizojengeka amani na si
mara zote kufanyika nchi zenye misuguano, vita na mivutano ya kisasa,
kijamii na kisiasa.
“Nchi nyingine hukuti haya yakifanyika,
huko ni migogoro, mivutano na hasama, hapa tumshukuru Mungu kwa kuwepo
na maelewano, umoja na mshikamano wetu,” alisema Balozi Seif.
Akimzungumzia Sheikh Ponda kutokana na hotuba zake, alisema zilikusudia
kuigawanya Zanzibar katika vipande vya uchochezi na chuki kwa nia ya
kuleta mgawanyiko.
Aidha, Balozi Seif aliwaonya wananchi
kutomuunga mkono mtu wa aina hiyo na kuwatahadharisha kuwa kama
yangetokea machafuko Sheikh Ponda asingepoteza ndugu wala jamaa visiwani
Zanzibar.
“Ponda hana jamaa wala ndugu hapa, si Pemba wala Unguja,
uchochezi wake ungeleta vifo na maafa, angesimama kando na kuwacheka
Wazanzibari, huyu ni mkaanga mbuyu,” alisema Balozi Seif.
Aliwataka watu kuacha kuonyesha CD za mihadhara yake na kwamba kufanya
hivyo kunaweza kuendeleza kupanda chuki na mgawanyiko miongoni mwa
Wazanzibari na wenzao wa Bara.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema Zanzibar haina upungufu wa wasomi wa
elimu ya dini za Kikristu na Kiislamu, hivyo kitendo cha kuja Ponda na
kuhamasisha chuki hakikubaliki na kutakiwa kulaaniwa.
PONDA NI MCHOCHEZI?????
Vuai
alisema Zanzibar ina hazina kubwa ya wasomi wenye upeo na ujuzi mkubwa
wa masuala ya dini, kwani masheikh wake ndio waliofanya kazi kubwa ya
kuzifikisha dini zote hadi Kigoma.
SHEIKH
PONDA NI MCHOCHEZI?????
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, amesema Katibu Mkuu wa Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda ni mchochezi sugu mwenye nia ya kumwaga sumu ili kuvuruga misingi ya amani na utulivu nchini.
Balozi Seif alitoa kauli hiyo juzi baada ya kupata futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya UVCCM katika ukumbi wa Gymkhana, kisiwani Unguja.
Alisema dhifa za mashirikiano na udugu hufanyika kwenye nchi zilizojengeka amani na si mara zote kufanyika nchi zenye misuguano, vita na mivutano ya kisasa, kijamii na kisiasa.
“Nchi nyingine hukuti haya yakifanyika, huko ni migogoro, mivutano na hasama, hapa tumshukuru Mungu kwa kuwepo na maelewano, umoja na mshikamano wetu,” alisema Balozi Seif.
Akimzungumzia Sheikh Ponda kutokana na hotuba zake, alisema zilikusudia kuigawanya Zanzibar katika vipande vya uchochezi na chuki kwa nia ya kuleta mgawanyiko.
Aidha, Balozi Seif aliwaonya wananchi kutomuunga mkono mtu wa aina hiyo na kuwatahadharisha kuwa kama yangetokea machafuko Sheikh Ponda asingepoteza ndugu wala jamaa visiwani Zanzibar.
“Ponda hana jamaa wala ndugu hapa, si Pemba wala Unguja, uchochezi wake ungeleta vifo na maafa, angesimama kando na kuwacheka Wazanzibari, huyu ni mkaanga mbuyu,” alisema Balozi Seif.
Aliwataka watu kuacha kuonyesha CD za mihadhara yake na kwamba kufanya hivyo kunaweza kuendeleza kupanda chuki na mgawanyiko miongoni mwa Wazanzibari na wenzao wa Bara.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema Zanzibar haina upungufu wa wasomi wa elimu ya dini za Kikristu na Kiislamu, hivyo kitendo cha kuja Ponda na kuhamasisha chuki hakikubaliki na kutakiwa kulaaniwa.
PONDA NI MCHOCHEZI????? |
Vuai alisema Zanzibar ina hazina kubwa ya wasomi wenye upeo na ujuzi mkubwa wa masuala ya dini, kwani masheikh wake ndio waliofanya kazi kubwa ya kuzifikisha dini zote hadi Kigoma.
No comments:
Post a Comment