Thursday, 8 August 2013

MFANYABIASHARA WA TANZANITE AUAWA KINYAMA...Erasto Msuya

 
 
 
 
 
 
MFANYABIASHARA WA
 TANZANITE AUAWA KINYAMA
Add caption

Habari zilizotufikia hivi punde Kutoka chumba chetu cha habari zinaeleza kuwa mmoja wa Wafanyabiasha wakubwa wa Madini jijini Arusha aliyejulikana kwa jina la

Erasto Msuya, aliyekuwa mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa madini ikiwemo TANZANITE na mmiliki wa SG HOTEL (Pichani) iliyoko Arusha, amepigwa risasi zaidi ya sita na watu wasiojulikana na kufa papo hapo. Polisi walipofika eneo la tukio walikuta mwili wa marehemu ukiwa hatua chache kutoka kwenye gari lake aina ya Range Rover.

Marehemu Erasto alikuwa akitokea KIA kwenda BOMA ambako alikuwa ameitwa na watu (ambao hawakujulikana mara moja) ili wakafanye biashara.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi-Amen.

No comments:

Post a Comment