Ofisa Uhamiaji wa Kituo cha Rusumo, Samweli Mahirane amethibitisha kuwa
hadi sasa zaidi ya Wanyarwanda 500 kutoka katika maeneo mbalimbali
ndani na nje ya Ngara wamevuka mpaka kurejea makwao kutii agizo la
Mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Kikwete la kuwataka wahamiaji haramu warejee
makwao kwa hiari au wafuate taratibu za kuhalalisha uhamiaji wao kndani
ya muda alioutoa.
Mahirane alisema wahamiaji hao wanatokea
katika vijiji vya Wilaya za Ngara, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Geita
pamoja na Runzewe na wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo bila vibali
halali.
“Kuondoka kwa hiari kwa wahamiaji haramu,
kutahitimishwa Jumatatu Agosti 12 na baada ya tarehe hiyo, vyombo vya
dola vitaanza kufanya kazi kama agizo la Rais Kikwete lilivyoelekeza
katika Mikoa ya Kagera na Kigoma,” alisema Mahirane.
Ofisa Uhamiaji wa Kituo cha Rusumo, Samweli Mahirane amethibitisha kuwa hadi sasa zaidi ya Wanyarwanda 500 kutoka katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Ngara wamevuka mpaka kurejea makwao kutii agizo la Mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Kikwete la kuwataka wahamiaji haramu warejee makwao kwa hiari au wafuate taratibu za kuhalalisha uhamiaji wao kndani ya muda alioutoa.
Mahirane alisema wahamiaji hao wanatokea katika vijiji vya Wilaya za Ngara, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Geita pamoja na Runzewe na wamekuwa wakiishi katika maeneo hayo bila vibali halali.
“Kuondoka kwa hiari kwa wahamiaji haramu, kutahitimishwa Jumatatu Agosti 12 na baada ya tarehe hiyo, vyombo vya dola vitaanza kufanya kazi kama agizo la Rais Kikwete lilivyoelekeza katika Mikoa ya Kagera na Kigoma,” alisema Mahirane.
No comments:
Post a Comment