Thursday, 15 August 2013

DK. MGIMWA : SERIKALI KUCHUNGUZA HOSPITALI BINAFSI

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 DK. MGIMWA : SERIKALI KUCHUNGUZA
 HOSPITALI BINAFSI


 
 
 
Photo: DK. MGIMWA : SERIKALI KUCHUNGUZA HOSPITALI BINAFSI

Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa amesema Serikali iko katika mpango wa kuzifanyia uchunguzi hospitali binafsi zinazotoa huduma ya afya kwa gharama kubwa ingawa zinapata misamaha ya kodi mbalimbali zinapoagiza dawa na vifaa vingine vya afya.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Fedha,  Dk. William Mgimwa (pichani), alipotakiwa na waandishi wa habari kutoa msimamo wa serikali kuhusu hospitali binafsi zinazotoza fedha nyingi kwa wagonjwa.

Dk. Mgimwa alisema baada ya uchunguzi huo Serikali itachukua hatua madhubuti dhidi ya Serikali kwani ilitarajiwa kuwa kusamehewa kodi kungewanufaisha wananchi kwa kupata matibabu kwa gharama nafuu.Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa amesema Serikali iko katika mpango wa kuzifanyia uchunguzi hospitali binafsi zinazotoa huduma ya afya kwa gharama kubwa ingawa zinapata misamaha ya kodi mbalimbali zinapoagiza dawa na vifaa vingine vya afya.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa (pichani), alipotakiwa na waandishi wa habari kutoa msimamo wa serikali kuhusu hospitali binafsi zinazotoza fedha nyingi kwa wagonjwa.

Dk. Mgimwa alisema baada ya uchunguzi huo Serikali itachukua hatua madhubuti dhidi ya Serikali kwani ilitarajiwa kuwa kusamehewa kodi kungewanufaisha wananchi kwa kupata matibabu kwa gharama nafuu.

No comments:

Post a Comment