RC TANGA AMUWEKA MAHABUSU
MKAGUZI WA NDANI
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni Mtaafu Chiku Gallawa, amemuweka rumande
Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Najim Mpate, kwa
madai ya kumdharau wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Tukio
hilo lilitokea jana wakati Mpate alipokuwa anatoa maelezo kufuatia hoja
za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Halmashauri ya
Pangani ambapo ilionekana kuna hoja ambazo hazijapatiwa majibu tangu
mwaka wa fedha 2008/2009.
Hoja
kuu inayoongelewa ni ile inayohusu mkandarasi mmoja aliyelipwa fedha
zaidi ya mkataba ulivyokuwa unaonyesha hivyo Mkuu wa Mkoa alikuwa
anataka maelezo kwa nini hoja hiyo ya karibu miaka mitano iliyopita
inaendelea kujirudia na kwanini mkandarasi husika hajarudisha fedha hizo
ili kufuta hoja hiyo.
Mara baada ya kujieleza Mkaguzi huyo
alilipiga chini kabrasha alilokuwa amelishinda, kitendo ambacho
kiliwashtua madiwani kwani kilionekana kuwa ni dharau ya wazi kwa Mkuu
wa Mkoa.
Baada ya tukio hilo, hilo Mheshimiwa Gallawa alisikika
akisema, “Hivi huyu ni nani mbona amekaa kijeuri. Kwanza unajibu
maswali kijeuri, lakini mimi ni mtu wa kunitupia faili chini” Hii ni
halmashauri yako? OCD mchukue huyu mtu ukampumzishe.”
Akieleza baada
ya kuisha kikao, Mheshimiwa Gallawa alisema yeye ndiye anawajibika
HAlmashauri zinapokuwa na hoja zilizokosa majibu na hivyo hatakubali
wazembe wachahce kwenye halmashauri wamharibie dhamana aliyopewa ya
kuwatumikia wananchi.”
RC TANGA AMUWEKA MAHABUSU
MKAGUZI WA NDANI
Mkuu wa mkoa wa Tanga, Luteni Mtaafu Chiku Gallawa, amemuweka rumande Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Najim Mpate, kwa madai ya kumdharau wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Tukio hilo lilitokea jana wakati Mpate alipokuwa anatoa maelezo kufuatia hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Halmashauri ya Pangani ambapo ilionekana kuna hoja ambazo hazijapatiwa majibu tangu mwaka wa fedha 2008/2009.
Hoja kuu inayoongelewa ni ile inayohusu mkandarasi mmoja aliyelipwa fedha zaidi ya mkataba ulivyokuwa unaonyesha hivyo Mkuu wa Mkoa alikuwa anataka maelezo kwa nini hoja hiyo ya karibu miaka mitano iliyopita inaendelea kujirudia na kwanini mkandarasi husika hajarudisha fedha hizo ili kufuta hoja hiyo.
Mara baada ya kujieleza Mkaguzi huyo alilipiga chini kabrasha alilokuwa amelishinda, kitendo ambacho kiliwashtua madiwani kwani kilionekana kuwa ni dharau ya wazi kwa Mkuu wa Mkoa.
Baada ya tukio hilo, hilo Mheshimiwa Gallawa alisikika akisema, “Hivi huyu ni nani mbona amekaa kijeuri. Kwanza unajibu maswali kijeuri, lakini mimi ni mtu wa kunitupia faili chini” Hii ni halmashauri yako? OCD mchukue huyu mtu ukampumzishe.”
Akieleza baada ya kuisha kikao, Mheshimiwa Gallawa alisema yeye ndiye anawajibika HAlmashauri zinapokuwa na hoja zilizokosa majibu na hivyo hatakubali wazembe wachahce kwenye halmashauri wamharibie dhamana aliyopewa ya kuwatumikia wananchi.”
No comments:
Post a Comment