Wednesday, 14 August 2013

Mamlaka ya Maji Tanga yapewa agizo maalumu



Mamlaka ya Maji Tanga

 yapewa agizo maalumu




Tanga.Bodi mpya ya Mamlaka ya Majisafi na Maji taka jijini Tanga (Uwasa) jana ilizinduliwa rasmi na kutakiwa iongeze ufanisi ili iendelee kuwa miongoni mwa Mamlaka bora za mfano mzuri nchini.
Bodi hiyo itaongozwa wa Salum Shamte ambaye ni Mwenyekiti baada ya kuchukua nafasi ya Raymond Mhando ambaye aliiongoza tangu Agosti mwaka 2010 hadi Juni 2013.
Akizungumza wakati akizindua bodi hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego alisema bodi hiyo mpya ina jukumu la kuhakikisha inaimarisha majukumu yaliyoachwa na bodi iliyomaliza muda wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwasa, Joshua Mgeyekwa alisema wakati wa hafla hiyo kuwa Mamlaka hiyo ni bora na ya mfano nchini ambapo inatoa huduma ya majisafi kwa wakazi 262,398 ambao ni asilimia 96 ya wakazi wote wa Jiji la Tanga.
Kwa upande wa huduma ya majitaka Mamlaka hiyo inahudumia watu 26,520 ambao ni asilimia 9.7 ya wakaz.

No comments:

Post a Comment