Majambazi wavamia kituo
kikuu cha Polisi Mwanza
Wizi huo wa ajabu ulitokea Julai 18,
mwaka huu, ambapo majambazi hao walivunja kituo hicho ambacho ndani yake kuna
Ofisi ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC).
Mwanza. Majambazi wamevunja ofisi za Makao Makuu ya Polisi
Mkoa wa Mwanza na kuiba mali mbalimbali vikiwemo vielelezo vya watuhumiwa walio
na kesi mahakamani.
Wizi huo wa ajabu ulitokea Julai 18,
mwaka huu, ambapo majambazi hao walivunja kituo hicho ambacho ndani yake kuna
Ofisi ya Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC).
I.G.P..MWEMA |
Taarifa zilizolifikia gazeti hili
zilibaini kuwa majambazi hao walivunja ghala la vielelezo vya washtakiwa,
chumba cha ghala la vipuri vya magari ya polisi, zikiwemo ofisi za Wapelelezi
wa Makosa ya Jinai na Waendesha Mashtaka.
Majambazi hao wanadaiwa kuiba
majalada ya kesi, begi lililokuwa na vielelezo vya washtakiwa, kompyuta ndogo
mbili (Laptop) za ushahidi na kutoweka.
Wizi huo uliotokea usiku na
kubainika asubuhi, ambapo watu hao ambao idadi yao haijajulikana wanadaiwa
waliweza kufanikiwa kuingia ndani ya ofisi hizo za polisi, kwa kuvunja
madirisha mawili ya chumba cha ghala la ofisi za Mkaguzi wa Elimu Kanda ya Ziwa
ambazo zinapakana na Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati cha Jijini Mwanza, kisha
kufanikisha wizi huo.
Habari zilizopatikana kutoka ndani
ya Jeshi la Polisi zinaeleza kwamba wizo huo ambao ulilenga ofisi ya vielelezo
na mashtaka, ulipangwa kwa umakini na kutekelezwa bila ya polisi waliokuwa zamu
usiku huo kubaini lolote.
Kwa mujibu wa maelezo wezi hao
inadhaniwa ni watu wenye uzoefu na jengo hilo, wakiwa na nia ya kuchukua
vielelezo mbalimbali pamoja na mafaili muhimu ya kesi kubwa.
Hili ni tukio lingine kubwa kutokea
kwa Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza sambamba na tukio la kuuawa kwa aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, Oktoba 13, mwaka jana
ambaye alipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi saa nane usiku
wakati akitoka katika kikao cha harusi.
Kauli ya Kamanda Mangu:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,
Evarist Mangu, amethibitisha kutokea kwa wizi huo na kusema jeshi lake
linafanya uchunguzi wa kina kubaini waliohusika, na kusisitiza kuwa kama ni
askari wake ama watu toka nje hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Alisema wezi hao waliingilia katika
ofisi ya Ukaguzi Elimu Kanda ya Ziwa ambako walivunja madirisha mawili, moja
likiwa ni kuingia ndani ya ghala la ofisi za elimu na dirisha lingine la
kutokea nje ya ghala hilo, kisha kuvunja dirisha la ndani ya majengo ya polisi
na kufanikisha wizi huo.
“Wezi hao walipiga jeki nondo za
madirisha hayo, hivyo kung’oka na kuingia ndani kisha kwetu, walianza kuingia
katika ghala la polisi la kuhifadhia vifaa vya ofisi vya Jeshi la polisi,
lakini inaonekana walikosa cha kuiba, huko walipanda darini na kutokea katika
chumba kingine nako hawakuiba, lakini katika chumba cha vielelezo ambako
walikuta begi lililokuwa na nguo za vielelezo pamoja na kompyuta ndogo mbili,
Lap Top, ambazo walitoweka nazo,” alieleza Kamanda Mangu.
Chumba kingine kinachodaiwa kuvunjwa katika wizi huo ni chumba kinachotunza
vipuri vya magari vilivyotumika, ambako Kamanda alidai kuwa hakuna kilichoibwa
pamoja na chumba cha vielelezo walikochukua begi la vielelezo.Mkaguzi wa Elimu Kanda:
Kwa upande wake kaimu Mkaguzi wa Elimu Kanda ya Ziwa, Florencia Vicent, alisema wao hawakugundua wizi huo kutokana na chumba kilichovunjwa kuwa ni ghala, ambacho hakifunguliwi kila mara na kwamba hakikuwa na vitu zaidi ya milango mibovu na maboksi tupu.
“Asubuhi mkaguzi mwenzangu alinieleza kamba wamefika polisi hapa na kudai tumeibiwa hivyo tuliamua kufungua stoo yetu na kuangalia, ambapo tulibaini kuvunjwa kwa madirisha hayo mawili pamoja na dari, lakini inaonekana kama walikuwa wakitafuta njia ya kuingilia na kutoka polisi baada ya wizi,” alieleza mkaguzi huyo.
Alisema ndani ya ghala lao waliweza kukuta suruali mbili mpya moja ikiwa ni aina ya jinsi na nyingine kadeti vikiwa vimetelekezwa ambapo polisi walivitambua kama ni sehemu ya vielelezo vyao na kuondoka navyo.
“Hapa tunaye mlinzi lakini, analinda eneo la ofisi zetu, eneo ambako wezi wameingia lipo chini ya polisi na lina mlango ambao hutumika kupitishia mahabusu, huko wapo polisi, hivyo inaonekana kwetu hakuna kitu kilichoibiwa, mpaka sasa tumefanya ukaguzi wa kina lakini hatuna kitu ambacho kimeibiwa, walengwa katika wizi huo ni polisi na hapa ilikuwa kama njia,” alifafanua kaim
No comments:
Post a Comment