Tuesday, 16 July 2013

TAARIFA YA POLISI

TAARIFA YA POLISI KUHUSU KUHOJIWA KWA MH. MBOWE 

Advera Senso-SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso-SSP, imetoa taarifa kuwa tarehe 15 Julai, 2013 majira ya mchana, Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe alijisalimisha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, kufuatia tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikimkabili zikiwemo kauli za uchochezi ambazo amekuwa akizitoa dhidi ya Jeshi la Polisi, Vyombo Vingine vya dola na Serikali kwa ujumla.
Jeshi la Polisi nchini, linaendelea kumhoji Mhe. Mbowe juu ya kauli hizo ambazo zimekuwa na mlengo wa uchochezi na kuijengea jamii taswira hasi juu ya vyombo vya ulinzi na usalama na kuwafanya wananchi kuwa na hofu.
Aidha, uchunguzi wa kina unaendelea na pindi itakapothibitika kuhusika kwake ama mtu mwingine yeyote kutoka ndani au nje ya chama cha CHADEMA hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Majambazi yateka mabasi mawili

IGP Sais Mwema 
  Jumanne,Julai16  2013  saa 11:49 AM
Kwa ufupi
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema majambazi wapatao kumi waliokuwa na silaha nzito za kivita asubuhi ya Jumatatu waliteka mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakielekea katika majiji ya Arusha na Dar es Salaam.

IGP Sais Mwema
Kagera. Kundi la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wameteka mabasi mawili ya abiria na kufanya uporaji katika Pori la Hifadhi ya Biharamulo Mkoani Kagera na kupora bunduki aina ya SMG iliyokuwa na askaRi aliyekuwa anasindikiza mabasi hayo.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema majambazi wapatao kumi waliokuwa na silaha nzito za kivita asubuhi ya Jumatatu waliteka mabasi mawili ya abiria yaliyokuwa yakielekea katika majiji ya Arusha na Dar es Salaam.
Alisema silaha zilizoonekana eneo la tukio ambazo zilitumiwa na majambazi kujihami ni SMG sita na LMG mbili.
Kwa mujibu wa Kalangi, mabasi yaliyotekwa ni NBS lililokuwa likielekea Arusha na RS lililokuwa likielekea Dar es Salaam,ambapo kabla waliteka gari dogo na kulitumia kufunga barabara katika hali iliyoonekana lilikuwa limeharibika.
Katika tukio hilo, abiria mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Fredrick Rugaihura (47)mkazi wa mjini Bukoba alijeruhiwa shingoni kwa risasi, ambapo majambazi hao walipora mali mbalimbali za abiria zikiwemo fedha na simu.

No comments:

Post a Comment