Blantyre. Rais wa Malawi, Joyce Banda amewaambia Marais wa zamani wa Msumbiji na Afrika Kusini hakuna cha kuzungumza kuhusiana na mzozo wa Ziwa Nyasa.
Joachim Chissano na Thabo Mbeki walikwenda Lilongwe kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mzozo wa mpaka wa Malawi na Tanzania.
Nchi hizo mbili ziliuwasilisha mzozo huo kwa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika(Sadc), ambayo kwa sasa
iko chini ya Chissano.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema: “Wao [Chissano
na Mbeki] walikwenda Malawi kwa mazungumzo hayo sasa tunasubiri
watakapokuja, tutazungumza.”
Katika mkutano wa kwanza uliofanyika Tanzania,
mawaziri wa mambo ya nje walifikia muafaka wa kukubaliana
kutokukubaliana kuhusu suala hilo na kuliwasilisha kwa viongozi wa
zamani wa Sadc kwa ajili ya maridhiano.
Rais Banda alimwambia Chissano pia kuwa katika
majadiliano hayo, endapo Malawi itaona hairidhishwi na mwenendo wa
majadiliano, italipeleka suala hilo mahakama za kimataifa.
No comments:
Post a Comment