Uwanja wa Soweto....wawaka moto
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia
(FFU) pamoja na askari kutoka Chuo cha Mafunzo ya Polisi (CCP) Moshi wakiwa
kwenye Uwanja wa Soweto, Arusha kuwadhibiti waombolezaji waliofika kwa ajili ya
kutoa heshima za mwisho kwa watu watatu waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa
bomu uliotokea Jumamosi iliyopita. Picha na Filbert Rweyemamu
Kubwa zaidi ni kifo cha mtoto Amir Ally (7) anayedaiwa kupigwa risasi na polisi. Maelezo ya kifo cha Ally yamenukuliwa kutoka kwa mtoto mwenzake Abubakar Adam (11), ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru akiuguza majeraha yanayodaiwa kutokana na risasi.
Jumamosi ya Juni 15, 2013 Jiji la
Arusha kwa mara ya pili ndani ya kipindi kifupi liliendelea kuandika historia
ya hatari kwa kutokewa na vitendo vya kigaidi. Vitendo vya kurusha mabomu
kwenye mikusanyiko ya watu na kusababisha maafa.
Tukio la kwanza lilitokea Mei 5,
2013, katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasit mjini
Arusha na kusababisha vifo vya watu watatu. Tukio hilo kwa sasa kesi yake iko mahakamani.
Hata hivyo tukio la Jumamosi
iliyopita lilitokea kwenye Uwanja wa Soweto mjini Arusha wakati wa mkutano wa
kukamilisha kampeni za udiwani wa Chadema. Wasiwasi mkubwa ulizuka katika tukio
hilo ni kuhusishwa polisi na vifo vilivyotokea.
Kubwa zaidi ni kifo cha mtoto Amir
Ally (7) anayedaiwa kupigwa risasi na polisi. Maelezo ya kifo cha Ally
yamenukuliwa kutoka kwa mtoto mwenzake Abubakar Adam (11), ambaye amelazwa
katika Hospitali ya Mount Meru akiuguza majeraha yanayodaiwa kutokana na
risasi.
Licha ya hao wawili, Kaimu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Arusha Medical Lutheran Center (ALMC), Dk Paul
Kisanga aliwataja watoto wengine wawili ndugu Fatuma na Sharifa Jumanne ambao
wamepelekwa Nairobi, Kenya, kwa matibabu zaidi baada ya miili yao kukutwa na vyuma.
Dk Kisanga alimtaja mtoto mwingine
Fahad Jamal (7) ambaye yuko chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu
(ICU), akisubiri timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili.
Kwa mujibu wa Dk Kisanga watoto hao
watano walipatwa na matatizo hayo wakati wakitoka madrasa eneo la Kaloleni
(Madrasa ni shule zinatoa elimu ya dini ya Kiislamu), iliyopo jirani na Uwanja
wa Soweto.
Tukio la Soweto limekuwa na matukio
mawili ndani yake; kwanza ni tukio la kurushwa bomu ambalo mtuhumiwa wake hajafahamika,
tukio la pili ni matumizi ya silaha za moto ambazo sababu za matumizi yake na
wahusika bado ni kitendawili.
Hata hivyo, mashuhuda wa tukio hilo
akiwamo mtoto Amir Ally wanadai polisi walipiga risasi watu, wengine wanakwenda
mbali zaidi kwa kudai kuwa mtuhumiwa wa bomu hilo alionekana akisafirishwa na
gari pale wananchi walipotaka kumvamia.
Wakuu wa polisi kwa upande wao
wamekiri kupatikana kwa maganda ya risasi katika eneo la tukio, hii ina
maanisha kwamba ni kweli ndani ya tukio la ulipuaji bomu kulikuwa na tukio
lingine la ufyatuaji risasi. Lakini bado hakujawa na ushahidi wa moja kwa moja
kwamba nani alifyatua risasi na kwa sababu gani. Madai ya kufyatulia risasi
watoto yana uzito wa pekee, pamoja na kutokuwepo kwa ushahidi wa moja kwa moja,
vidole vingi vimekuwa vikinyooshwa kuwatuhumu polisi, kwamba risasi
zilizofyatuliwa eneo la tukio zilitoka kwa polisi, na watoto walipigwa risasi
na polisi.
Hata hivyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi,
Inspekta Jenerali Said Mwema tayari ameunda timu ya askari polisi kuchunguza
tukio hilo ambalo polisi wanatuhumiwa.
Kwanza tuweke wazi kwamba tuna imani
kubwa na utendaji kazi wa Jeshi Polisi, hivyo maoni yetu ni katika kujenga
nyumba moja kwa maana tukio la Soweto kwa watoto kupigwa risasi linahitaji Tume
Huru itakayokuwa na kada mbalimbali za wataalamu.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia
(FFU) pamoja na askari kutoka Chuo cha Mafunzo ya Polisi (CCP) Moshi wakiwa
kwenye Uwanja wa Soweto, Arusha kuwadhibiti waombolezaji waliofika kwa ajili ya
kutoa heshima za mwisho kwa watu watatu waliopoteza maisha kwenye mlipuko wa
bomu uliotokea Jumamosi iliyopita. Picha na Filbert Rweyemamu
Kubwa zaidi ni kifo cha mtoto Amir Ally (7) anayedaiwa kupigwa risasi na polisi. Maelezo ya kifo cha Ally yamenukuliwa kutoka kwa mtoto mwenzake Abubakar Adam (11), ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mount Meru akiuguza majeraha yanayodaiwa kutokana na risasi.Tunaamini kuwa hata kama tume iliyoundwa na Mwema itafanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa, bado hali ya wasiwasi itaendelea kuwapo kwa kuwa polisi wananyooshewa kidole karibu na watu wengi. Ni vyema Serikali ingeunda Tume Huru.
No comments:
Post a Comment