Thursday, 20 June 2013

Saida Karoli yu hai ....mwenye chuki ajinyonge



Saida Karoli
Nipo mzima, mtaanza kwanza nyie kufa wazushi

 Mana Bukoba wakumbwa na kiwewe baada ya kusikia kipenzi wao wa mkoa wa kagera Saida Karoli kaaga dunia.....walipuka kwa furaha baada ya kusikia yeye mwenyewe akikanusha uzeshi huo...




Utamaduni wa mtanzania
MWIMBAJI wa muziki wa asili nchini, Saida Kalori, amezushiwa kifo, huku mwenyewe akilizungumzia hilo kwa kusema kuwa wanaotaka afe wataanza wao kwanza.


Saida Karoli, pichani
Taarifa hizo zilianza kuzagaa usiku wa juzi na kuzua hofu kwa wadau wa muziki Tanzania, ukizingatia kuwa tayari kumekuwa na mfululizo wa vifo vya wasanii, akiwapo Albert Mangweha ‘Ngwair, Langa Kileo na wengineo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mbeya Vijijini, mwimbaji huyo wa Mapenzi Kizungu zungu, Chambua Kama Karanga na nyinginezo, alisema kuwa
habari za kifo chake ni za uzushi na zimelenga kuwachanganya wapenzi wake Tanzania na duniani kwa ujumla.



Alisema kuwa sio kweli kama amekufa kama habari hizo zilivyotolewa, hivyo wanaotaka afe wataanza wao kwanza kabla yake.

“Sio kweli kuwa nimekufa, hivyo wadau waelewe kuwa nipo salama, huku Mbeya vijijini,”

alisema Saida na kuzipinga kwa nguvu zote habari hizo zinazosema kuwa amefariki kwa ajali ya boti na wengine kudai kuwa amepata ajali ya gari.

Saida anaheshimika kwa nyimbo zake nyingi zilizomuweka katika kilele cha mafanikio ya muziki hapa nchini, akiimba zaidi nyimbo za asili ya Bukoba na kujizolea mashabiki lukuki.

Tunakuombea maisha marefu mama SAIDA KALOR

I


No comments:

Post a Comment