GENERALI WA JESHI ALIYEFICHUA SIRI
RAIS AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA!!!
Jenerali
wa Jeshi aliyesababisha hali ya mshikemshike au sekeseke nchini Uganda wakati
maudhui ya barua aliyoiandika yalipofichuka hadharani amezungumza na BBC kwa
mara ya kwanza.
Generali David Sejusa, mmoja wa maafisa wa juu katika
jeshi la Uganda alitaka kufanyike uchunguzi wa tuhuma kuwa kuna mpango wa
kuwaua maafisa waandamizi wa jeshi na
“Wa serikali wanaopinga kile kilichotajwa kuwa ni mradi
wa Muhoozi, mtoto wa Rais Museveni akiandaliwa kumrithi baba yake.”
Magazeti mawili na vituo vya Radio vilifungwa
kwa karibu siku kumi wakati maafisa usalama walipokuwa wakijaribu kutafuta
barua hiyo.
Tangu barua hiyo ilipotolewa hadharani,
Jenerali huyo amekuwa kama yuko mafichoni.
Sejusa anasema kuwa yeye ndiye aliyendaika
barua hiyo ila hafahamu vipi ilifika mikononi m,wa vyombo vya habari.
Aidha Sejusa amelaani hatua ya serikali
kushambulia vyombo vya habari baada ya barua hiyo kufichuliwa akisema kuwa yeye
ndiye alikuwa mwandishi wa barua yenyewe na kuwa serikali ingemsubiri arejee
Uganda ndiposa iweze kumhoji kuhusu maudhui ya barua hiyo.
Akizungumza na BBC Swahili, Jenerali Sejusa
alisema tatizo kubwa na kitu ambacho anakipagia Uganda ni kutaka kuweka muda
ambao rais anapaswa kutawala nchio hiyo. Amelaani uongozi wa Rais Yoweri
Museveni akisema kuwa katiba ya nchi inapaswa kulindwa kwa njia yoyote labda
hata kutumia nguvu dhidi ya wale wanaoikiuka.
“Hata hivyo Serikali ya
Uganda imepuuzilia mbali madai hayo ya
Jenerali David Sejusa.
Akizungumza na BBC, msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo, amesema madai
hayo hayana msingi wowote.
Aidha amesema Uganda
inatawaliwa kwa misingi ya katiba ya nchi hiyo na ikiwa Jenerali huyo ana
malalamiko ya kikazi au kiutawala anaweza kutumia njia ambazo zimewekwa na
katiba ya Uganda. Chanzo: bbcswahili”
No comments:
Post a Comment