Bomu lililotumika
imetengenezwa China
Arusha. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema bomu lililolipuliwa katika mkutano wa Chadema ni la kijeshi na limetengenezwa China.
Akizungumza mjini hapa jana, Pinda alisema uchunguzi unaendelea kujua
bomu hilo limefikaje kwenye mikono ya waliohusika kwani uzoefu
unaonyesha kuwa hutumiwa na wanajeshi kujihami wakiwa katika makabiliano
na maadui vitani.
“Ingawa uchunguzi unaendelea, lakini inawezekana bomu hilo
limeingizwa nchini na wahalifu wasiojulikana kupitia njia za panya za
mipakani,”
alisema Pinda.
alisema Pinda.
Serikali kusimamia mazishi
Katika hatua nyingine, Serikali imetangaza kwamba itasimamia mazishi ya watu waliopoteza maisha kutokana na shambulio hilo.
Hatua hiyo imekuja huku Chadema nacho kikiwa kimetangaza
kushughulikia mazishi ya wananchi hao kwa kuwa walifariki katika
shambulio lililotokea kwenye mkutano wao.
Waziri Mkuu, jana alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo
kusimamia shughuli zote za misiba hiyo, agizo ambalo wadadisi wa masuala
ya kisiasa wanasema ni kama kuipokonya Chadema dhamana ya kusimamia
shughuli za mazishi hayo.
Juzi jioni, Mbowe aliwaambia wananchi na wafuasi wa Chadema katika
Viwanja vya Soweto kuwa chama chake kitagharimia na kusimamia shughuli
zote za kuaga, kusafirisha pamoja na mazishi ya waliopoteza maisha
katika tukio hilo.
Chama hicho tayari kilishafunga mahema katika Viwanja vya Soweto kwa
ajili ya shughuli hiyo, lakini uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha
Mikutano cha Arusha (AICC), kilizuia kuendelea kwa shughuli hiyo hali
iliyosababisha machafuko.
No comments:
Post a Comment