Ø Rais wa Rwanda, Paul Kageme, amewaonya viongozi wa vyama vya
upinzani, wanaotarajiwa kurejea nchini humo juma hili kutoka Ubelgiji. Kagame
amewataka viongozi hao, akiwemo waziri mkuu wa zamani, Faustin Twagiramungu,
wawe waangalifu akisema Rwanda haiko tena jinsi walivyoiacha miaka mingi
iliyopita. Viongozi hao wanasema wanakwenda Rwanda kuvisajili vyama vyao,
lakini mmoja wa waasisi wa vyama hivyo yuko gerezani Kigali. Je
kweli demokrasia inafanya kazi Rwanda?

Afya ya rais wa zamani
wa Afrika Kusini Nelson Mandela imeanza kuimarika baada ya siku kadhaa kuwa katika
hali mbaya. Je umuhimu gani aliyo nao Nelson Mandela kwako wewe na kwa maisha
yako?
No comments:
Post a Comment