Mkoa wa Tanga
Mkoa wa Tanga | |
Nembo ya Tanzania | |
Mahali pa Mkoa wa Tanga katika Tanzania | |
Anwani ya kijiografia: 5°0′S 38°15′E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 6 |
Mji mkuu | Tanga |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | Mizengo K. P. Pinda |
Eneo | |
- Mkoa | 27,348 km² |
Idadi ya wakazi (2002) | |
- Mji | 1,642,015 |
Tovuti: http://www.tanga.go.tz/ |
Yaliyomo |
Eneo la mkoa
Mkoa una eneo la 27,348 km² na uko Kaskazini Mashariki mwa Tanzania ukipakana na Kenya upande wa Kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki na mikoa ya Morogoro, Manyara na Kilimanjaro. Mpaka upande wa kusini unafuata mto wa Mligaji.Kuna wilaya 8 ambazo ni Lushoto, Korogwe, Muheza, Mkinga, Handeni, Kilindi, Pangani na Tanga Mjini. Eneo linalofaa kwa kilimo ni 17,000 km². Tanga ni kati ya mikoa midogo ya Tanzania ikiwa na msongamano mkubwa wa wakazi ndani ya eneo lake.
Wilaya za Mkoa wa Tanga
|
||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Ramani | Wilaya au manisipaa | Wakazi (2002) | Tarafa | Kata | Kijiji | Eneo km² |
Wilaya ya Handeni | 393,931 | 13 | 23 | 102 | 13,209 | |
Wilaya ya Korogwe | 261,004 | 4 | 20 | 132 | 3,756 | |
Wilaya ya Lushoto | 419,970 | 8 | 32 | 137 | 3,500 | |
Wilaya ya Muheza | 279,423 | 6 | 27 | 140 | 4,922 | |
Wilaya ya Pangani | 44,107 | 4 | 13 | 23 | 1,425 | |
Tanga mjini | 243,580 | 4 | 21 | 23 | 536 | |
Jumla | 1,642,015 | 37 | 136 | 557 | 27,348 | |
Wilaya ya Handeni imegawanywa kuwa wilaya mbili za Handeni na Kilindi; Muheza iligawiwa kuwa wilaya mbili za Muheza na Mkinga |
||||||
Marejeo: Mkoa wa Tanga |
Wakazi
Makabila makubwa mkoani Tanga ni Wasambaa, Wazigua, Wabondei na Wadigo. Wasambaa ndio kabila kubwa lililoko katika milimani ya Usambara, Muheza, Korogwe na Lushoto. Kwa jumla ndio asilimia 40 ya wakazi wote wa mkoa.Wazigua ni kabila kubwa huko Handeni na sehemu za Korogwe na Pangani. Wabondei wako hasa Muheza na sehemu za Pangani. Wadigo ndio wengi Tanga penyewe na sehemu za Muheza.
Msongamano wa wakazi ni mkubwa hasa wilaya ya Lushoto penye ardhi yenye rutuba nzuri. Wiyala ya handeni kuna machimbo ya madini.ila kuhusu elimu ipo nyuma sana.kwani mpaka sasa hakuna shule ya sekondari inayotoa huduma ya kidato cha tano na sita.kama haitoshi shule za watu binafsi hakuna ata moja
Hali ya hewa
Kwa jumla hali ya hewa ni joto lenye unyevu. Handeni kuna joto ikiwa pakavu zaidi. Milima ya Usambara hapana joto sana. Miezi ya Desemba - Machi halijoto huko Tanga inafikia sentigredi 30-32 mchana na 26-29 usiku. Wakati wa Mei hadi Oktoba halijota inapoa ni sentigredi 23-28 mchana na 20-24 usiku. Unyevu iko juu kati ya asilimia 100 na asilimia 65.Maeneo mengi ya mkoa hupokea angalau milimita 750 za mvua kwa mwaka au zaidi. Pwani ni zaidi takriban milimita 1,100 hadi 1,400 mm ikipungua sehemu za ndani isipokuwa milima ya Usambara ambako mvua inaweza kuzidi milimita 2000 kwa mwaka.
Uchumi
Wakazi wengi hutegemea kilimo cha riziki pamoja na ufugaji na uvuvi. Mazao ya chakula hasa ni mahindi, muhogo, ndizi, maharagwe na mpunga.- Mazao ya biashara ni katani, pamba, kahawa, chai, nazi, tumbaku na korosho.
- Mifugo ni ngombe, mbuzi na kondoo pamoja na kuku.
- Katani ilikuwa zao la biashara hasa kwa ajili ya Tanga tangu kuingizwa kutoka Mexico zamani za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Hulimwa kote mkoani isipokuwa Lushoto, hasa Muheza na Korogwe kwenye mashamba makubwa. Mashamba haya yalikuwa ya walowezi, yalitaifishwa baada ya uhuru. Tangu kuanguka kwa sekta ya umma yamebinafsishwa tena siku hizi. Zao la katani inategemea sana soko la dunia, umuhimu wake ilirudi nyuma tangu miaka ya 1960.
Utalii umeanza kupanuka kidogo hasa katika eneo la Pangani,Mapango ya Amboni na kituo cha Makumbusho URITHI Tanga.
Viungo vya nje
- (Kiingereza) Tanga Region Socio-Economic Profile (PDF)
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
No comments:
Post a Comment