Monday, 1 July 2013
MFALME Mswati III wa Swaziland,
MFALME Mswati III wa Swaziland, leo anafungua rasmi Maonesho ya 37, ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba(DITF), yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara ya Nje nchini (TanTrade), Jacqueline Maleko alisema maonesho hayo yatafunguliwa badala ya tarehe ya awali iliyokuwa Julai 4, mwaka 2013.
Alisema maonesho hayo yatafunguliwa saa tatu asubuhi katika viwanja hivyo na kuwaomba washiriki na wananchi kuwahi kwenye viwanja hivyo ili kufanya ufunguzi huo ufane na kuleta picha halisi ya maonesho.
Akizungumzia maonesho hayo, Maleko alisema ni ya kipekee kwa mwaka huu kwa kuwa yana mvuto na yameboreshwa zaidi huku nchi za nje zinazoshiriki zikiwa 32 pamoja na kampuni za nje 400.
No tags for this post.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment