Mapambano dhidi ya
Boko Haram mipakani
Serikali ya Nigeria imetuma kikosi kikubwa cha wanajeshi pamoja na silaha kukabiliana na wapiganaji katika majimbo matatu ya Kaskazini Mashariki mwa nchi.
Taarifa kutoka kwa serikali ilisema kuwa nia ya kutumwa kwa wanajeshi hao ni kuweza kupata tena udhibiti wa sehemu ambazo inaaminika ziko chini ya udhibiti wa wapiganaji hao, pamoja na kuimarisha usalama
Mnamo Jumanne Rais Goodluck Jonathan, alitangaza hali ya hatari, katika majimbo matatu ya Yobe, Borno na Adamawa baada ya majimbo hayo kushuhudia mashambulizi mabaya sana.
Wapiganaji kutoka kundi la Boko Haram,
wanalaumiwa kwa kufanya mashambulizi hayo.
Kundi hilo ambalo lina mizizi yake Kaskazini mwa Nigeria,limehusishwa na mauaji ya watu 2,000 tangu mwaka 2010.
Boko Haram, limedhibiti baadhi ya sehemu za kaskazini mwa nchi, kwa miaka mitatu iliyopita na nyingi ya ghasia wanazofanya zimekuwa sana sana katika eneo hilo.
Hakuna shaka kuwa hali Kaskazini mwa Nigeria inaendelea kuzorota na sasa rais Goodluck Jonathan amekiri hilo. Hakuna yeyote serikali angeweza kulitamka hilo.
Ukubwa wa mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram, umelazimisha rais Jonathan kuchukua hatua na hata kuwanyamazisha baadhi ya wakosoaji wake wanaosema kuwa amejikokota kuchukua hatua.
Baadhi ya wadadisi wamependekeza kuwa ikiwa hali itaandelea kuzorota hivyo, itakuwa vigumu kukabiliana na kundi la Boko Haram na litaweza hata kuunda taasisi zake.
Je, wanajeshi zaidi wataweza kukabiliana na hali? kikubwa ni ambavyo wanajeshi hao wataendesha harakati zao.
Wadadisi wanasema kuwa , jeshi lina kibarua kigumu kwani kuna dalili tayari limeshindwa katika vita hivi, na raia wanahisi kuwa katikati ya mtego Nigeria
No comments:
Post a Comment