WALIOKUWA WANATAKA MUUNGANO WA
MKATABA WAANZA KUBABAIKA
Tume ya Mabadiliko ya KAtiba imeendelea kupokea maoni ya wajumbe wa
mabaraza ya Katiba huku hoja ya kuwepo kwa muungano wa mkataba
ikionekana kutokuungwa mkono na wajumbe wengi.
Wakitoa mawazo
yao kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Ecrotanal Kisiwani
Unguja chini ya Kamishna wa Tume Awadh Said Ali, wajumbe wa mabaraza ya
Katiba ya Wilaya walieleza kuwa wanaodai Serikali tatu, Muungano wa
mkataba au kuvunja muungano wana jazba ambazo ni hatari kwa uhai wa
visiwa vya Zanzibar.
Mjumbe
Khalid Salehe Mwina alisema “Muundo wa Serikali mbili ubakei,
haiwezekani mgonjwa aumwe mguu apasuliwe kichwa. Zanzibar eneo letu la
ardhi, ambayo ndio kimbilio la watu maskini kama sisi, ni dogo tofauti
na bara, tusijitenge na kushindwa kutumia fursa za kiuchumi zilizoko
bara.”
Idadi kubwa ya wajumbe walisema Serikali mbili
hazina matatizo kwa wananzi labda kwa viongozi waroho wa madaraka.
Isipokuwa walisisitiza kuwa kero za Muungano zinapaswa kushughulikiwa
kwa wakati. Hoja za wengi zilijikita katika uwezo ulioonyeshwa na
Serikali mbili katika kulinda amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
(Kwa habari mbalimbali tembelea : http://www.dar24.com/)
Tume ya Mabadiliko ya KAtiba imeendelea kupokea maoni ya wajumbe wa mabaraza ya Katiba huku hoja ya kuwepo kwa muungano wa mkataba ikionekana kutokuungwa mkono na wajumbe wengi.
Wakitoa mawazo yao kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Ecrotanal Kisiwani Unguja chini ya Kamishna wa Tume Awadh Said Ali, wajumbe wa mabaraza ya Katiba ya Wilaya walieleza kuwa wanaodai Serikali tatu, Muungano wa mkataba au kuvunja muungano wana jazba ambazo ni hatari kwa uhai wa visiwa vya Zanzibar.
Mjumbe Khalid Salehe Mwina alisema “Muundo wa Serikali mbili ubakei, haiwezekani mgonjwa aumwe mguu apasuliwe kichwa. Zanzibar eneo letu la ardhi, ambayo ndio kimbilio la watu maskini kama sisi, ni dogo tofauti na bara, tusijitenge na kushindwa kutumia fursa za kiuchumi zilizoko bara.”
Idadi kubwa ya wajumbe walisema Serikali mbili hazina matatizo kwa wananzi labda kwa viongozi waroho wa madaraka. Isipokuwa walisisitiza kuwa kero za Muungano zinapaswa kushughulikiwa kwa wakati. Hoja za wengi zilijikita katika uwezo ulioonyeshwa na Serikali mbili katika kulinda amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
(Kwa habari mbalimbali tembelea : http://www.dar24.com/)
No comments:
Post a Comment