Serikali yafafanua sababu
za kuzuia
magari ya utalii ya Kenya
Dar es Salaam. Serikali imeshtukia ujanja wa wafanyabiashara wa sekta ya utalii wa nchini Kenya wa kutaka waruhusiwe kuingia nchini na magari ya kubeba watalii yaliyosajiliwa nchini mwao.
Wakenya hao wanataka kutumia kisingizio cha ushirikiano wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kuingia Soko la Utalii Tanzania.
Mkurugenzi wa Utalii, Wizara ya Maliasili na
Utalii, Ibrahim Mussa alisema hayo jana wakati akijibu madai ya vyombo
vya habari vya Kenya kuwa Tanzania inawanyanyasa wafanyabiashara wake wa
sekta ya utalii wanapojaribu kuingia nchini.
Vyombo hivyo vya Kenya, juzi vilimnukuu Mkurugenzi
wa Shirikisho la Wenye Mahoteli na Huduma za Vyakula Pwani la nchini
humo, Sam Ikwaye akidai wafanyabiashara hao wanazuiwa kuingia kwenye
hifadhi nchini na magari yao yaliyobeba watalii.
Mussa alisema Kenya inataka kuiburuza Tanzania katika eneo hilo kutokana na ukweli kuwa makubaliano ya EAC hajafikia hatua hiyo.
“Kenya wanataka kushinikiza tuwaruhusu waingie
kufanyabiashara ya utalii nchini wakati suala hilo kwa ngazi ya EAC lipo
hatua ya kuangalia sera za kila nchi zinasemaje,”
alisema.
alisema.
Mkurugenzi huyo alibainisha kuwa baada ya hatua
hiyo ambacho kitafuata ni upitiaji wa sheria kabla ya kutunga mpya
ambazo zitaendana na mahitaji ya kila nchi na jumuiya kwa ujumla wake.
No comments:
Post a Comment