Unguja wakataa
Serikali tatu
Zanzibar. Wajumbe wa Baraza la Katiba Wilaya Kaskazini (B) Unguja wameukataa Muundo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania kwa madai kuwa utaliongezea taifa gharama zisizokuwa za lazima.
Wakizungumza wakati wa kutoa maoni yao kwenye
rasimu ya Katiba, Wajumbe hao hamesema hawaoni haja wala ulazima wa kuwa
kuliongezea taifa gharama hizo, wakati nchi bado ina mambo mengi
yanayohitaji uwezeshwaji.
Abdallah Kombo Baraka kutoka shehia ya Zingwe
zingwe akichangia alisema mfumo huo ambao ulipendekezwa na Tume haufai
kwa sasa hivi Taifa lina mambo yakushuhulikia kuliko kuongeza jukumu
lingine.
“Hivi sasa kupata huduma kume jaa urasimu halafu unaongeza Serikali ya tatu si hatari zaidi” alisema Baraka.
“Waheshimiwa hivi sasa uchumi wetu uko chini
halafu tunataka kuongeza Serikali ya tatu njaa si itatisha jamani, mimi
napendekeza muundo wa sasa uendelee” alisema Khamis Makame Mkombe
akichangia katika Mkutano huo.
Alisema kuleta Muungano wa shirikisho ni njiia za kuua Mungano ambao umedumu kwa nusu karine.
Sambamba na hayo Salim Suleiman Ameir kutoka
shehia ya Donge alisema Muundo wa serikali tatu si makubaliano ya
Waasisi Abeid karume na Mwalimu Nyerere na kudai kuleta mfumo mpya ni
kuvunja heshima yao.
“Tukiwa na Muungano wa shirikisho lazima kuwe na
mkataba maalumu mmoja akiukiuka ndio Muungano ushavunjika uoo, kwa hiyo
ni vyema tuendelee na mfumo wetu huu uliasisiwa na wazee wetu ili tupate
radhi zao” alieleza Ameir.
Baadaye Mjumbe wa tume ya mabadiliko katiba Awadhi
Ali Said alitoa ufafanuzi uliolenga kuelezea Serikali ziliopo Tanzania
lakini wajumbe hao waliendelea na msimamo wao huo.
No comments:
Post a Comment