Thursday, 25 July 2013

KIJIJI CHA KAKUNYU CHAPATA NEEMA YA MAJI

NEEMA KIJIJI CHA BUGANGO NA KAKUNYU





Wakati maji yalipo sindikama kupatikana kijijini Bugango wataalamu wa uchimbaji maji wakihamisha mitambo yao na kusema kwaherini tutarudi tena......(na kituachia kitendawili cha kusema BAHATI YA MTENDE UTAMU WA TENDEZAKE MWENYEWE) Leo mungu kakitegua kitendaweli hicho na yakaaji wa kijiji hicho kwa kusema 
"HAKUNA KINACHO SHINDIKANA KATIKA MIKONO YA MUNGU"


Eneo lenye ukame latatua kitendawali hiki cha uhaba wa maji 
katika vijiji hivi viwili vya Bugango na Kakunyu na eneo hili lipo maeneo ya Kitongoji  cha Bandama na Kitoboka katikati ya milima hiyo ya katangiliza na Nseseme....mwamba umepasuka na kububu jisha maji mengi mazuri na baridi Mkuu wa kanisa linalio pakana na chemichemi hiyo mbele yake akiri kwa kusema muaka yote tuna tabika kwa ajili ya upatikanaji wa maji sasa leo mungu ashusha miujiza yake kama hii katika ukame huu hapa ng'ombe wetu walidhoofika kwa kukosa maji sasa chanzo cha maji chajitokeza karibu na sisi hapa jangweni
 "MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU" alimalizia kwa maneno hayo.....






Kwakweli maji ni kitu muhumu sana kwa mahitaji ya mwanadamu ukikosa maji uhai haupo pale na Kamanda wa Uhamiaji wa eneo hili ali washauti wakaaji wa eneo hilo kukihifadhi chanzo hicha cha chemichemi hii kisije kikaharibiwa na mifugo ...na kushauri watengeneze mifereji itakayo tenganisha kwa matumizi ya majihayo na mifugo na binadamu...




Ng'ombe wakiwa malishoni na wakielekea kwenye eneo la kujipatia maji hayo yaliyo shushwa na Mungu.....WANANCHI WALIKUWA WAKIRUMBANA NA KUSEMA HAYA SI MAMBO YA KAWAIDA BALI HUENDA NI SALA ZETU TUNAZO MPELEKEA MUNGU NA LEO KAZISIKIA KWANI HAPA MAJI YALIKUWA ADIMU SANA dumu la maji lilifukia Shs/= za Kiganda 1,500/= hadi 2.000/=
NIVYEMA TUKAMSUFU MUNGU waliishia hapo na maBlioga wa Bogango Border, Boshazi, Kwetu Tanga, Zigua Simo na Njero wakiondoka katika kijiji cha maeneo ya Bandama na Kotoboka wakiwaacha wananchi wakishikwa na Butwaaaa.

No comments:

Post a Comment