Thursday, 20 June 2013

Saida Karoli yu hai ....mwenye chuki ajinyonge



Saida Karoli
Nipo mzima, mtaanza kwanza nyie kufa wazushi

 Mana Bukoba wakumbwa na kiwewe baada ya kusikia kipenzi wao wa mkoa wa kagera Saida Karoli kaaga dunia.....walipuka kwa furaha baada ya kusikia yeye mwenyewe akikanusha uzeshi huo...




Utamaduni wa mtanzania
MWIMBAJI wa muziki wa asili nchini, Saida Kalori, amezushiwa kifo, huku mwenyewe akilizungumzia hilo kwa kusema kuwa wanaotaka afe wataanza wao kwanza.


Saida Karoli, pichani
Taarifa hizo zilianza kuzagaa usiku wa juzi na kuzua hofu kwa wadau wa muziki Tanzania, ukizingatia kuwa tayari kumekuwa na mfululizo wa vifo vya wasanii, akiwapo Albert Mangweha ‘Ngwair, Langa Kileo na wengineo.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mbeya Vijijini, mwimbaji huyo wa Mapenzi Kizungu zungu, Chambua Kama Karanga na nyinginezo, alisema kuwa
habari za kifo chake ni za uzushi na zimelenga kuwachanganya wapenzi wake Tanzania na duniani kwa ujumla.



Alisema kuwa sio kweli kama amekufa kama habari hizo zilivyotolewa, hivyo wanaotaka afe wataanza wao kwanza kabla yake.

“Sio kweli kuwa nimekufa, hivyo wadau waelewe kuwa nipo salama, huku Mbeya vijijini,”

alisema Saida na kuzipinga kwa nguvu zote habari hizo zinazosema kuwa amefariki kwa ajali ya boti na wengine kudai kuwa amepata ajali ya gari.

Saida anaheshimika kwa nyimbo zake nyingi zilizomuweka katika kilele cha mafanikio ya muziki hapa nchini, akiimba zaidi nyimbo za asili ya Bukoba na kujizolea mashabiki lukuki.

Tunakuombea maisha marefu mama SAIDA KALOR

I


KWETU TANGA & BOSHAZI Blog...wawakaribisha ICT Officer's


BUGANGO BORDER:

wakipewa taarifa

picha ya pamoja

wakiwa ndani ya gari

wakisain kitabu cha mapokezi





BUGANGO BORDER:



BUGANGO BORDER: yatembelewa na wageni wa ICT –kitoka HQ Dar-Es salam Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa mawanza….na Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kagera wakagua Ofisi wajitambulisha wafurahia sana na kudai yakuwa Idara ya Uhamiaji ni kila kona ya Tanzania ….Pia viongozi wa Blog ya Boshazi na Kwetu Tanga wakishirikiana na Uongozi wa Bugango Border wapongeza sana ujio wao na kukiri ya kuwa safari yao ni changamoto kwa wana BUGANGO……
Ujimbe huo ulikuwa na watu wafuatao:-
*      MOHAMEDI AWESU…….SSIS (ICT) HQ-Dar es salaam,
*      ALI  A. ALI…………CBMM (AIIS) Mwanza,
*      RODERN L. MTULO…….ICT HQ DSM,
*      MABROUK A. KHAMIS………..ICT HQ DSM,
*      SAULO KASHEKE …….(MT),
*      ABDALLAH M NASSORO- BUKOBA

Ziara yao imetembelea Mkoa mzima wa Kagera Ulio na Ofisi za Uhamiaji na kukagua huduma zao za ICT….uongozi wa Bugango border ume wapokea na una wakaribisha tena mkoani kagera…


Wednesday, 19 June 2013

Bomu lililotumika





Bomu lililotumika 

imetengenezwa China




Arusha. Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema bomu lililolipuliwa katika mkutano wa Chadema ni la kijeshi na limetengenezwa China.
Akizungumza mjini hapa jana, Pinda alisema uchunguzi unaendelea kujua bomu hilo limefikaje kwenye mikono ya waliohusika kwani uzoefu unaonyesha kuwa hutumiwa na wanajeshi kujihami wakiwa katika makabiliano na maadui vitani.

“Ingawa uchunguzi unaendelea, lakini inawezekana bomu hilo limeingizwa nchini na wahalifu wasiojulikana kupitia njia za panya za mipakani,”

  alisema Pinda.
Serikali kusimamia mazishi
Katika hatua nyingine, Serikali imetangaza kwamba itasimamia mazishi ya watu waliopoteza maisha kutokana na shambulio hilo.
Hatua hiyo imekuja huku Chadema nacho kikiwa kimetangaza kushughulikia mazishi ya wananchi hao kwa kuwa walifariki katika shambulio lililotokea kwenye mkutano wao.
Waziri Mkuu, jana alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo kusimamia shughuli zote za misiba hiyo, agizo ambalo wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema ni kama kuipokonya Chadema dhamana ya kusimamia shughuli za mazishi hayo.
Juzi jioni, Mbowe aliwaambia wananchi na wafuasi wa Chadema katika Viwanja vya Soweto kuwa chama chake kitagharimia na kusimamia shughuli zote za kuaga, kusafirisha pamoja na mazishi ya waliopoteza maisha katika tukio hilo.
Chama hicho tayari kilishafunga mahema katika Viwanja vya Soweto kwa ajili ya shughuli hiyo, lakini uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), kilizuia kuendelea kwa shughuli hiyo hali iliyosababisha machafuko.