Tuesday 20 August 2013

JWTZ kushiriki mazoezi Angola

Simba wa Tanzania

JWTZ kushiriki mazoezi 

Angola




JWTZ...
Dar es Salaam. Maofisa na Askari 35 wa Jeshi la
Wananchi (JWTZ), kutoka Kamandi ya Jeshi la Anga wameondoka nchini jana kuelekea Angola kushiriki mazoezi ya kijeshi ya Blue Zambezi ambayo yanatarajiwa kuanza nchini humo leo (Agosti 20) hadi Agosti 31 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa kuwaaga maofisa hao katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam jana, Meja Jenerali Hassan Vuai Chema aliwataka wanajeshi hao kuonyesha nidhamu ili kujenga ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na nchi zingine za Jumuia ya Mandeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
JWTZ

“Mkiwa Angola mna jukumu la kufanya kazi kwa bidii, kujifunza na kutoa kwa wengine kile ambacho tunacho ili wengine wajifunze kutoka JWTZ” 

alisema Meja Jenerali Chema na kuongeza kuwa katika msafara huo kuna maafisa 21 na askari wa kawaida 14.
Alisema kuwa msafara huo utaongozwa na Brigedia Jenerali Azra Ndimgwango na mazoezi hayo yanashirikisha vikosi vya jeshi kutoka nchi zingine za SADC yakiwa na lengo la kuwaandaa wapiganaji hao kutoa msaada mara nchi moja inapotokewa na majanga.

“Tunawandaa wawe tayari yanapotokea majanga kama vile usambazaji wa chakula, dawa na vifaa vingine”

alisema na kuongeza kuwa mafunzo hayo ambayo yatahusiaha matumizi ya helikopta katika kukabiliana na majanga anaamini yatapanua zaidi upeo wa wanajeshi wa nchini katika kukabiliana na majanga.

kwetu Tanga

No comments:

Post a Comment