Thursday 22 August 2013

Fisi mawindoni....

 
 
Fisi Mawindoni
MANISPAA ILALA YASIMAMISHA WATENDAJI 
WAKE KWA UBADHIRIFU
Ubadhilifu Halimashauri

Baraza la Madiwani la Manispaa ya Ilala limewasimamisha kazi watumishi wanne wa Manispaa hiyo kwa vitendo mbalimbali vya ubadhirifu wa mali za umma pamoja na uwajibikaji usioridhisha.
Hatua hii imekuja baada ya Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kukataa kupokea taarifa za mapato na matumizi za Halmashauri ya Ilala baada ya kubaibni ubadhirifu wa zaidi ya shilingi bilioni 2/=. Aidha Baraza la Madiwani limeagiza watumishi wengine 21 kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Maamuzi hayo yalitangazwa na Meya wa Manispaa hiyo, Ndugu Jerry Silaa, ambaye aliwataja waliosimamishwa kuwa ni mhandisi wa Manispaa ambaye anatuhumiwa kwa kusimamia ujenzi na sheria za mipango miji. Tuhuma nyingine za Mhandisi huyo ni pamoja na kushindwa kusimamia ukarabati wa barabara mjini na matumizi yaayotia mashaka ya fedha za ukarabati wa barabara, kutoa kibali cha ujenzi wa ghorofa 14 katika mtaa wa Indira Gandhi wakati kwa mujibu wa sheria zilizopo eneo hilo inaruhusiwa kujenga majengo yasiyozidi ghorofa 10.

Mtumishi mwingine aliyesimamishwa ni Mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa majengo kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa majengo kwa mujibu wa sheria zilizopo. Aidha, anatuhumiwa kuchangia ajali ya jingo lililoanguka katika mtaa wa Indira Gandhi na kusababisha vifo vya watu 36 na wengine kujeruhiwa.
Aidha katika watumishi ambao Baraza la Madiwani limeagiza kuwa wachukuliwe hatua za kinidhamu ni pamoja na KAimu Ofisa elimu Sekondari na Kaimu Ofisa Elimu Msingi katika manispaa hiyo.
 
KETU TANGA
 

No comments:

Post a Comment