Wednesday 4 September 2013

Tanapa yawataka wananchi kulima mazao mbadala



Swala

Twiga

Simba
Pangani. Hifadhi ya Taifa Tanapa, imewataka wananchi waishio karibu na
hifadhi za wanyamapori nchini, kubadilika na kuacha tabia ya kuishi kimazoea badala yake wawe wabunifu kwa kupanda mazao ambayo hayashambuliwi na wanyama waishio katika maeneo ya mbuga za wanyama.
Meneja Ujirani Mwema Taifa, Ahmed Mbugi alisema endapo wakazi wa maeneo jirani watapanda mazao kama ufuta, pilipili za kuwasha pamoja na miti ya kutanda itasaidia kuzuia njia za wanyama kupita kwenye maeneo yao.
Hayo aliyasema wakati wa mafunzo ya uandishi wa masuala ya hifadhi yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini na Mazingira na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wilayani Pangani hivi karibuni.

Tanga Kwetu

Sunday 1 September 2013

Mkurugenzi wa Uhamiaji Rwanda azuru Tanzania

Tembo wa Tanzania

 
 
 

Wakuu wa idara za Uhamiaji wa Rwanda Na Tanzania

Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Tanzania, Mgnus Ulungi (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Uhamiaji Rwanda Kalibata Anaclet (Katikati) kuhusu masuala mbali ya uhamiaji wakati mkurugenzi huyo aliptembelea Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini, Dar es Salaam jana. (Picha na Uhamiaji)

Simba Jike na Dume