Saturday 27 July 2013

Mlandizi. Familia ya Amina Juma




Mlandizi. Familia ya Amina Juma, mjane wa askari wa JWTZ, Fortunatus Msofe aliyeuawa akiwa Darfur, nchini Sudan, imesema baada ya siku 40 tangu kufa kwa mpiganaji huyo, itatoa tamko kuhusu yaliyomsibu binti yao. Amina aliyekuwa akiishi Visiga mkoani Pwani na Msofe aliyezikwa juzi, Kange mkoani Tanga, alifungiwa nyumba waliyokuwa wakiishi na habari zilisema hatua hiyo ilitokana na amri ya baba mkwe wake, Wilbad Msofe.
Mzee Msofe alihamisha msiba kutoka Visiga na kupeleka nyumbani kwake Tanga, hatua iliyomlazimisha Amina kurejea kwao Mlandizi.
Hata hivyo, baadaye alikata shauri kwenda Tanga kumzika mwenza wake kwa maelezo aliota Msofe akimsihi aende akampumzishe.
Akizungumza nyumbani kwa wazazi wa Amina, jana mmoja wa wanafamilia alisema ndugu yako na mama yake mzazi walikwenda kwenye maziko.
Alisema baada ya kutoka kwenye msiba, Amina amekuwa mnyonge kwa sababu hakupata nafasi ya moja kwa moja ya kumzika mwenzake.

“Hapa kulikuwa na vikao kujadili msiba huo na kauli zilizotoka, wanandugu walikubaliana kuwa kwa sasa si vyema kujadili, hadi 40 itakapofika,” 
 alisema.

No comments:

Post a Comment