Monday 17 June 2013

NAWAJUZA


Ø  Rais wa Rwanda, Paul Kageme, amewaonya viongozi wa vyama vya upinzani, wanaotarajiwa kurejea nchini humo juma hili kutoka Ubelgiji. Kagame amewataka viongozi hao, akiwemo waziri mkuu wa zamani, Faustin Twagiramungu, wawe waangalifu akisema Rwanda haiko tena jinsi walivyoiacha miaka mingi iliyopita. Viongozi hao wanasema wanakwenda Rwanda kuvisajili vyama vyao, lakini mmoja wa waasisi wa vyama hivyo yuko gerezani Kigali. Je kweli demokrasia inafanya kazi Rwanda?



Ø  Nchi nne kati ya tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki, zikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda, zimeongeza kodi ili kutunisha fuko la bajeti la kila nchi jambo ambalo limezusha vilio kwa wananchi walio wengi katika mataifa hayo wakisema wanabebeshwa mzigo wasiostahili. Nchi ya tano mwanachama Burundi, huwa haitangazi bajeti katika tarehe sawa na nchi nyengine na mwaka huu inatarajiwa kuitangaza bajeti yake mwezi Desemba. Bajeti zilizosomwa zitaleta tija katika kuimarisha maisha ya wakaazi wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, huku Burundi ikichelewa kutangaza bajeti yake kila mwaka kwa mujibu wa katiba yake?

 

 Afya ya rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela imeanza kuimarika baada ya siku kadhaa kuwa katika hali mbaya. Je umuhimu gani aliyo nao Nelson Mandela kwako wewe na kwa maisha yako?

No comments:

Post a Comment