Saturday 21 September 2013

TANZIA

TANGA KWDETU

TANZIA

"Kwa ishirikiano wa Bliog za Tanga Kwetu, Zigua Simo na njero, Boshazi ondeZigua, Samba na Baragumu ya Mnyonge....wamestushwa na kifo cha Kamanda "


GEORGE JOHN LAIZER

 

Che.Andrew Kizenga Shundi

kwani Tarehe 17/09/2013 alitembelea BUGANGO BORDER na kuahidi yakuwa atakapo pata nafasi atatembelea eneo hili tena na kusema yakuwa alikuwa akisikia kituo hiki cha Bugango sasa leo amefika ...akasema kwakweli mimi siamini nitarudi tena....mwisho wa kauri yake kwakweli sisi wana bugango tunamuomboa apumzike mahali pema peponi..Amin

                      
                              

                                       



  • MPIGANAJI AFIA 'VITANI' AKILITETEA TAIFA LAKE
  • AMEACHA MKE NA WATOTO WAWILI.
  • AFISA UHAMIAJI MKOA WA KAGERA AONGOZA WAOMBOLEZAJI 
     
     
Idara ya Uhamiaji mkoa wa Kagera imekumbwa na simanzi na majonzi makubwa baada ya kumpoteza askari wake Mkaguzi wa Uhamiaji George John Laizer aliyefariki jana katika kituo cha Afya Bunazi wilayani Missenyi akisubiri matibabu. 
Marehemu Laizer alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ambapo inasemekana siku mbili kabla ya kifo chake alikuwa akiugua typhoid. Baada ya kwenda kituoni hapo kutibiwa hali yake ilibadilika ghafla jana asubuhi hali iliyopelekea akimbizwe kituo cha Afya kwa matibabu. Akiwa kituoni hapo, ndipo alipokata roho na kuiga dunia.
Marehemu Laizer ni mzaliwa wa mkoa wa Arusha mwaka 1970,  alipata elimu ya msingi  katika shule ya Mchombe mkoani Morogoro kuanzia mwaka 1979 hadi 1985. Mwaka 1986 hadi 1989 alipata elimu ya sekondari katika shule ya Vunjo.
Mnamo tarehe 12/12/1990, aliajiriwa rasmi kuwa afisa uhamiaji mara baada ya kumaliza mafunzo ya awali katika chuo cha polisi Moshi na kupangiwa kufanya kazi katika kituo cha Holili mkoa wa Kilimanjaro.
Marehemu ameacha mke na watoto wawili.Leo asubuhi mjini Bukoba katika ofisi za uhamiaji, Afisa Uhamiaji mkoa wa Kagera DCI. George Kombe aliongoza maofisa mbalimbali kutoka vyombo vya ulinzi na usalama na asasi za kiraia katika kuuaga mwili wa marehemu ambapo baadaye majira ya saa tano na nusu asubuhi ulisafirishwa kwenda Rusumo ambako huko pia ataagwa na hatimaye kusafirishwa nyumbani kwao mkoani Arusha kwa mazishi.
Blogu ya Bugango inaungana na wana-Uhamiaji katika wakati huu mgumu wa kuomboleza kuondokewa na kijana aliyekufa akilitumikia taifa lake katika oparesheni Kimbunga.
 
Askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wakitoa heshima zao za mwisho kwa Kamana Laizer leo hii mjini Bukoba                                      
 
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN
Mlima kilimanjaro
 

No comments:

Post a Comment